MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TAIFA ABDURAHMANI KINANA AWATAKA. WANAVYUO. NCHINI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI


Na  Sheila Ahmadi



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa rai kwa vijana kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo ili kuongeza vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi.CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa rai kwa vijana kujitokeza wa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo ili kuongeza vijana katika nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi.


Hayo  yamesemwa jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Kanali Abdulrahman Kinana katika mkutano Mkuu maalumu wa ukaribisho wa Wananchama wapya 1,167 seneti ya vyuo vikuu tawi la DIT, CBE, IFM na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kutoka tawi la Kibasila kata ya Upanga Mashariki.


Amesema Chama kitajitahidi kuwapitisha vijana kwa wingi kwenye kugombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya mtaa.


“Chama kinawategemea sana vijana kwani ndio chachu ya mawazo ya Chama hivyo wasifikiri kuwa kuna sehemu nyingine mawazo yatatoka hivyo watambue kuwa wao ni taifa la leo.Amesema Kinana.



” Kutokana na hilo mnao uwezo mkubwa wa kutushauri , kitujenga na kutukosoa tunawategemea sana, toeni mawazo, mwaka huu tuna Uchaguzi wa serikali za Mitaa, nawasihi vijana wa vyuoni jitokezeni na gombeeni kwa nafasi zote mwaka huu,” amesema. Kinana


Aidha. Mwenyekiti kinana  amesema kuwa  Chama hicho ni kikubwa hivyo wanapaswa kukilinda, kujipanga,kuweka mikakati na kugawa majukumu.

Kutokana na mambo yanayochangia kukipa ushindi Chama hicho kuwa ni utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM, hivyo amewataka vijana hao kuchagua viongozi wenye uwezo sio wa kubebwa wala kutumia fedha kupata nafasi kwani Hata Rais Dk.Samia ameahidi hakuna mtu atakayebebwa bali atachaguliwa kutokana na sifa zake.

Naye ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu amesema katika kuhakikisha seneti imaweza kusimama yenyewe na kujitegemea Ofisi ya mkoa watachangia sh.milioni 2 kwenye mfuko wa vijana zitakazochangia kununua vitu vitakavyowawezesha kujitegemea.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema wanatarajia wanachama hao wapya ambao ni wasomi wataenda kuyasemea mambo mazuri yanayofanywa na Rais Dk.Samia.

“Hatua hii inaonyesha jinsi Rais Dk.Samia anavyofanya vizuri na kugusa nyoyo za Watanzania hivyo sasa Ilala tunaanza rasmi ajenga ya Samia ya mwaka 2025 kuleta ushindi na ushindi ni lazima”Amesema Zungu.

Ameongeza kuwa katika chaguzi zinazotarajiwa 2024/2025 watambeba na kumtetea kiongozi anayesimamia umoja wa Watanzania na kubeba kero zao.

“Msibabaishwe wala msidanganywe na wasiokitakia mema Chama chetu na nchi yetu, hivyo Jimbo la Ilala tutachangia sh.milioni tano ili muweza kujisimamia na pia mikopo inayotewa na serikali msizubae mjiimarishe kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu wasiostahili kuchukua mikopo,” amesema.

Zungu amewataka vijana hao kuachana na vitu vya anasa, vitakavyowapoteza muda bali watumie mitandao kufanyabiashara zao ili kujiongezea kipato.

Katika hatua nyingine , Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amempongeza Kinana Kwa kuwa mlezi mzuri wa vijana na jinsi anavyofanya kazi anawapa nguvu ya kuendelea kuchapaka kazi. 


“Hali ya siasa kwa wilaya ya Ilala na mkoa wa Dar es Salaam ni mzuri hivyo tunashukuru Kwa kuwa na viongozi wa Chama Wazuri na wachapakazi na juhudi zako kama mlezi wa vijana zinazidi kutuongezea hamasa ya kuchapa kazi,” Amesema Mpogolo.

Vilevile , Katibu wa Seneti vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam, Mabula Mabula amemuomba mwenyekiti wa chama hiko Rais Dkt Samia Suluhu kuangalia namna ya kuwaongeza mikopo wanafunzi wa vyuo vya kati lakini pia kupata vitendea kazi ili waweze kujitegemea ambapo amevitaja vifaa hivyo ni compyuta,printer na mashine ya fotokopi.




Post a Comment

0 Comments