Na. sheila Ahmadi
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa nafasi mbalimbali za uongozi na kutoa fursa nyingi za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa wanachama hao kutokana na kuwa kinara wa kuhamasisha Chama kufika mbali katika kujiimarisha kimaendeleo
Hayo yamesemwa. jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi Taifa, Joran Lwehwbura Bashange Mara baada ya kuzungumza na Wanahabari Huku akitangaza zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho kuanzia feb 14 hadi 24 mwaka huu.
Mwenyekiti. Bashange amesema kuwa katika kutangaza nafasi mbalimbali ambazo zinagombewa ndani ya chama hicho ni pamoja na viongozi wakuu wa kitaifa ambapo ni Kiongozi wa Chama, Mwenyekiti Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa Tanzania Bara pamoja na Makamu Mwenyekiti Taifa Tanzania Zanzibar huku wajumbe wa Halmashauri Kuu ikiwa ni nafasi 24 na ujumbe wa kamati Kuu ni nafasi 24.
"Kwa upande wa Ngome wanawake Taifa, ni nafasi ya Mwenyekiti wa ngome ya wanawake Taifa, Makamu Mwenyekiti, Ujumbe wa Halmashaur Kuu Taifa nafasi 2, Ujumbe Mkutano Mkuu Taifa nafasi 2, huku upande wa Ngome Vijana Taifa ni nafasi ya Mwenyekiti wa ngome ya vijana Taifa, Makamu Mwenyekiti Taifa, Ujumbe halmashauri Kuu Taifa nafasi 2 na Ujumbe wa Mkutano Mkuu nafasi 2" amesema Bashange.
Hivyo kwenye , utaratibu wa kuchukua fomu na kurejeshwa itakua ni Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Magomeni Dar es Salaam, Vuga Zanzibar, Ofisi za mikoa na majimbo yote ya ACT Tanzania nzima huku watakao chukua fomu wakitakiwa kufika na stakabadhi ya malipo ambayo ni bank slip inayoonyesha wamefanya malipo kupitia akaunt ya Chama.
Vilevile , ameongeza kuwa wale wagombea wa Ngome ya vijana na wazee wanaporejesha fomu waambatanishe na nyaraka zinazoonesha uthibisho wa umri wao pamoja na picha 2 za passport size wakati wa kurejesha fomu.
Sanjari na hayo amesema kuwa pamoja na mambo mengine kutakuwa na mdahalo wa watia nia wa uenyekiti Ngome ya vijana feb 20, Uenyekiti gome Wanawake feb 27 pamoja na wagombea wa nafasi ya kiongozi wa chama na Mwenyekiti wa chama Taifa na Makamu wenyeviti Bara na zanzibar March 4, 2024.

0 Comments