TANI 1500 ZA SUKARI ZAWASILI NCHINi


Na. sheila  Ahmadi


Tani 1500. Za sukari  zawasili nchini  Tanzania ambapo kupitia serikali ya Awamu ya sita imeweza kuleta sukari kwa wananchi ili  kuweza kupunguza changamoto ambayo ilikuwa chachu kipindi cha nyuma  hivyo sukari hiyo inaenda kusambazwa mikoa mbalimbali nchini ikiwemo. Mtwara, Dar es salaam,  na Ruvuma .


Hayo yamesemwa Jjijini Dar esa laam  na Mkurugenzi wa Bodi ya sukari Tanzania  Profesa Kenneth  Bengesi   Mara baada alipotembelea bandarini  kwenye mapokezi ya sukari  kutoka kwenye Meli ya Kamapuni itwayo Yokohama Star ambapo amesema kuwa sukari hiyo iende kwa wananchi  hivyo baadhi ya wafanyabishara  wanatakiwa kuuza bei elekezi ambayo serikali inatambua.


Kwa kushirikiana na serikali bodi ya sukari imeweza kufanya kazi kwa wakati katika kwenda kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwani kipindi cha nyuma sukari ilikuwa ni chagamoto kupatikana kautokana hali ya hewa kutokua vizuri zaidi hivyo kwa sasa sukari tumepokea za kutosha kutoka nchi za nje na zinaenda kuuzwa kwa wafanyabishara.


"Mamlaka ya bandari imekuwa ikitusaidia Mara kwa Mara kwenye kupokea mizigo ya sukari hiyo meli hiyo imeweza kushusha kontena  55 hivyo inajumuisha na ile ambayo iliweza kutangulia Tani 3500 pia kuna meli nyingne ambayo itakuja Hivi karibuni hivyo tunaona sukari inaenda kuongezeka kwa kiasi kikubwa.


Tunasisitiza kuwa sukari ambayo imeingia ni  msamaha wa ongezeko la kodi na ongezeko la thamani kutoka kwenye serikali ili iweze kuwanufaisha watanzania wote nchini hivyo itakua jambo la kuhuzunisha iwapo wafanyabiashara wachache  wataachiwa katika kujinufaisha kwa sukari hii ambayo imeweza kuingia na ile ambayo inazalishwa ndani wakapandisha bei tutawachukulia hatua za kisheria na watakaopandisha bei isiyo halali. " Amesema Mkurugenzi Bengesi"


Kuna watu wanfikiri kua sukari ambayo inazalishwa ndani inatakiwa kuuzwa bei elekezi hiyo sio sahihi sukari inayozalishwa  ndani ya nchi na hii ambayo tumepokea kutoka nje inatakiwa ziuzwe bei moja elekezi kutokana na msingi wa uwekaji bei elekezi ilikuwa ni sukari ambayo inazalishwa kutoka ndani ya nchi ndio sababu sukari ambayo inatoka nje ya nchi inaonekana bei yake kua huu kidogo Huku serikali imeridhia kutoa msamaha wa kodi was ongezeko la Thamani na kushusha ili iweze kufanana na sukari ambayo inazalishwa nchini.


Naye   Meneja wa Ugavi kutoka  kampuni ya kilombero  sukari  Dickson luwumba  Sukari amesema sukari ambayo imeingia nchini. Inaenda kugawa kwa mawakala wetu wa sukari nchini hivyo tunahakikisha wateja wote waweze kupata sukari kufikia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ongezeko la sukari litakuwa kwa wingi  na kupelekwa katika mikoa yote nchini.


"Sisi kama kampuni ya kilombero sukari  tunajitahidi kwa hali na Mali katika kutoka huduma na bei elekezi ambayo imetolewa na bodi hiyo Huku wasambazaji, na Mawakala wetu wanaendelea kusambaza huduma hiyo ya sukari hivyo Tunaishukuru bodi ya sukari Tanzania kwa kuweza kupambania suala hilo la sukari kwani kipindi cha nyuma sukari ilikuwa chanagamoto  kwa wananchi.




Post a Comment

0 Comments