WABUNGE WA. AFRIKA MASHARIKI. (EALA) WAELEZA CHANGAMOTO YA UCHELEWESHWAJI WA MIZIGO BANDARINI. DAR ES ALAM



Na: Sheila  Ahmadi 


Wabunge wa  kamati ya Mawasisliano ,biashara,na uwekezaji  Afrika Mashariki.  (  EALA) wametembelea katika bandari ya Dar es salaam ambapo wamesema kuwa licha ya kuwa na mazingira wezeshi bado kuna chanagamoto  ya  ucheleweshwaji. Wa mizigo. Ambao unasababisha rushwa na gharama kubwa kwa wafanyabishara

.Akizungumza jijini Dar es salaam. mwenyekiti   wa wafanyabiashara kutoka Rwanda Rutazana Francine amesema kuwa tumekuja nchini Tanzania kukutana na wadau, wafanyabishara na maofisa forodha ili tuweze kujadili kazi za bandari ambazo zinaenda kuchangia kwenye ukuaji wa Uchumi.

"Sisi kama wabunge na wafanyabiashara tumeridhishwa na utendaji kazi wa bandari hiyo lakini bado tumeona kuna changamoto. Mbalimbali ambazo zinaweza kutatuliwa kwa wakatii na kufika malengo mahususi katika kupunguza changamoto hizo ambazo zinakuwa kero kwa wafanyabiashara.

Mwenyekiti   Rutazana aliongeza kwa kusema kuwa mahitaji ya bandari ni muhimu kwani wafanyabishara walio wengi hutumia bandari  kwa kusafirisha bidhaa kutoka nje ya nchi na ndani hivyo suala la malalamiko kuhusu kuchelewa kwa mizigo lifanyiwe kazi kwa uharaka zaidi "Amesema Mwenyekiti  Rutazana 

Naye mjumbe David. Ole sankok amesema Tanzania bado Ina maeneo mengi ya uwekezaji. Kwenye uchumi wa bluu kutokana na uwepo wa vyanzo Vingi vya maji vikiwemo ziwa Nyasa, Victoria hivyo vyanzo hivyo vinaenda kuleta mapato ya nchini na uendelezaji wa uchumi.

Katika ziara hii inaenda kupelekea Miundombinu ya uwekezaji ili kuweza kuleta sera ambazo zinaenda kuleta ongezeko madhubuti kupitia kwenye bandari   na kuweza kusafirisha bidhaa kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji kutoka bandari ya dar es salam Mussa biboze amesema kuwa bandari hii Ina uwezo kufanya kazi  kwa umahiri zaidi  na kuhakikisha kuwa mizigo inayotoka nje inashushwa kwa Wakati  maalumu. 

Baadhi ya changamoto kwenye bandari yetu zippo lakini tunaenndelea  kuzitatua hivyo maafisa wa forodha wanaendelea kutoa huduma zote katika usafirishaji wa mizigo na kupokea hivyo wafanyabishara kutoka mataifa mengine tunawakaribisha katika bandari yetu ya Dar es Salaam Amesema mkurugenzi mtendaji Biboze.






Post a Comment

0 Comments