Na Sheila Ahmadi
Bodi ya Wahandisi nchini yaadhimisha miaka 21 ya utendaji kazi ikiwa na lengo mahususi ya kuweza kuhamasisha wahandisi wadogo ambao wako vyuoni na kuwaanda vyema katika mafunzo mbalimbali ya kazi za uhandisi nchini .
Akizungumza jijini Dar esalaam mara baada ya mafunzo ya wahandisi wadogo Msajili wa bodi ya usajili Wahandisi Tanzania. Mhandisi Benard kavishe amewataka. Wahandisi ambao wanatoka vyuoni kabla ya kupata ajira wawe na uwezo wa kufanya kazi wenyewe na kusimamia miradi ambayo wamepewa hususani kwa miaka mitatu.
"Adha chama cha wanawake. Wahandisi Tanzania wamepewa majukumu katika msaada ule wa norway kwa ajili ya kuendeleza masomo ya Sayansi. Huku tukiendelea kufanya mafunzo kwa wale ambao ni wanufaika hivyo tumefanya mafunzo ya watu Takribani 500 kwa wale ambao wapo kwenye mradi na ambao hawapo kwenye mradi
Kuna baadhi ya watu wamedandia kwenye mradi huo katika kufanya mafunzo hayo huku tukitoa pongezi kwa wadau wetu wote kwani bila wadau jambo hilo lisingeweza kufanyika hivyo ni lazima kupata sehemu ambazo zitakua wezeshi kwenye utendaji wake na tumepata nafasi. Ya kuchakata wadau kwa ajili ya kuwashukuru. " Amesema Mhandisi kavishe"
Hata hivyo mbegu ya uhandisi inatakiwa kupandwa mapema kuanzia kidato cha kwanza na pili kwani inapofika kidato cha pili baadhi ya wanafunzi wanajigawa kwenda sanaa na sayansi hivyo tunakiwa kuandaa watoto wakiwa wadogo kwani uhandisi unatakiwa umahiri katika kujifunza hivyo kwa wale walioko sekondari na sana ndoto ya kuwa wahandisi lazima waendelee kusoma masomo ya sayansi, hesabu na fizikia.
Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa Mradi huo Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha maji Mhandisi. Nancy. MNduma ameongeza kusema kuwa mimi ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo hivyo nawashukuru bodi ya usajili wa wahandisi nchini kwa kuweza kuadhimisha miaka 21 programu ya cip ambayo mimi kama mnufaika wa programu hii ya mwaka 2018_ 2021 imekuwa muhimu kwa wahandisi ambao wanatoka vyuoni na kupitia mafunzo maalumu.
Kupitia mafunzo haya tumeweza kupata ujuzi mkubwa ambao unakuwezesha kwenda nje ya nchi kushiriki miradi mbalimbali ya kujenga Taifa hivyo ujuzi binafsi unaweza kutoka nao kwenye shughuli ambazo unaweza kufanya huko nje pÃa kukujengea uwezo wa mitandao ya kutoka mbali




0 Comments