Na sheila Ahmadi
Mamlaka ya kudhibiti mkondo wa juu wa Petroli PURA wametiliana saini ya makubaliano na Chuo cha bahari Dar es salaam (DMI) kwaajili ya kutoa mafunzo ya usalama kwa watu watakaofanya kazi katika shughuli zautafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta baharini.
Hayo yamesemwa mara baada ya Hafla ya utiaji saini Hiyo ambayo inahusu mashirikiano ya mafunzo katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia Mkurugenzi mkuu wa PURA Charles Sangweni amesema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kupunguza gharama wanazoziingia katika kuwafundisha wataalamu nje ya nchi.
" utafiti uliofanyika, watanzania hulazimika kutumia takriban Dola za Marekani 7,000 kushiriki mafunzo hayo nje ya nchi kwa muda wa siku tano. Fedha hizo zinajumuisha gharama za mafunzo, usafiri wa ndege, malazi, chakula, bima ya afya
Kutokuwepo kwa chuo kinachotoa mafunzo tajwa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla kunawalazimu watanzania wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi katika miradi inayotekelezwa baharini kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa kusomea kozi hizo. "Hii ni changamoto kubwa kwa kuwa watanzania wachache ndio wanaoweza kumudu gharama za kwenda nje ya nchi kusoma kozi husika".
"Hati hii inaenda kuweka msingi wa mashirikiano kati ya PURA na DMI katika kuwezesha uanzishwaji wa kituo chenye ithibati kitakachotoa mafunzo ya usalama na kujihami (accedited safety and survival training centre) kwa watanzania wanaofanya na wanaotarajia kufanya kazi maeneo ya baharini wakati wa utekelezaji wa shughuli za mafuta na gesi asilia".
Aidha ameongeza kuwa Azma ya PURA na DMI ya kuwezesha uanzishwaji wa kituo kitakachotoa mafunzo ya usalama na kujihami ni miongoni mwa hatua za makusudi ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Serikali kuongeza ushiriki wa watanzania katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.
Hivyo Miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni Offshore Petroleum Industry Training Organization (OPITO) na Basic Offshore Safety Induction and Emergency Training (BOSIET).
kufikia Februari, 2024, jumla ya futi za ujazo trilioni 57.54 za gesi asilia zimegunduliwa. Kati ya kiasi hicho, futi za ujazo trilioni 10.406 zimegunduliwa maeneo ya nchi kavu na kina kifupi cha bahari na futi za ujazo trilioni 47.13 zimegunduliwa katika maeneo ya kina kirefu cha bahari.
Naye Mkuu wa chuo cha DMI,Dkt. Tumaini S. Gurumo amesema shughuli zote za baharini zinahitaji usalama kwanza hivyo ni muhimu watu wanaojihusisha na maswala ya bahari kupatiwa mafunzo hayo kabla.
"Shughuli za uchimbaji wa mafuta na gesi zinazofanyika baharini zinauhitaji mkubwa tena naweza kusema wa ziada wa juu ya mafunzo ya usalama baharini ukizingatia huko hakuna hospital".
Ametoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa za uwekezaji katika shughuli za uchimbaji na utaftaji wa mafuta na gesi ilinkuongeza wigo wa ajila kwa watanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya PURA Halfani Halfani amesema taasisi zetu zinatekeleza kwa vitendo azima ya serikali ya kuongeza ushiriki wa watanzania katika shughuli za utafutaji,uchimbaji na uendelezaji wa miradi ya gesi.
Mwenyekiti wa Bodi ya DMI Kapteni Ernest Bupamba amesema shughuli za uchimbaji na utaftaji wa mafuta na gesi zinahitaji umakini mkubwa kwani uzembe wowote ukijitokeza unaweza kughalimu mradi mzima na ukizingatia kuwa miradi hiyo hutumia gharama kubwa.
0 Comments