Na Sheila Ahmadi
Chuo cha bahari Dar es salaam (DMI) Limeandaa kongamano kubwa la kimataifa linalohusiana na uchumi wa bluu mwezi julay mwaka huu ambapo, kongamano hilo linaenda kuhudhuriwa na Mataifa mbalimbali likiwemo Taifa la Ghana litaweza kushiriki katika kongamano hilo hivyo kupitia uchumi huo wa bluu utaenda kuleta fursa kwa watanzania katika kukuza uchumi na kuwapa elimu ya kutosha kuhusu uchafuzi wa bahari.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa chuo cha bahari Dar es salaam DMI Dkt Tumaini Gurumo alipozungumza Na wanahabari ambapo amesema kuwa mkutano huo unaenda kufanyika tarehe tatu mpaka nne lengo ikiwa ni kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusiana na bahari kwani ni muhimu kutoa mafunzo ili kufika kwenye uchumi wa bluu ambapo nchi yetu inaenda kujulikana kimataifa kutokana na bahari zetu ambazo tunazo nchini.
"Kongamano letu ambalo tunaenda kulifanya ni la uchumi wa bluu ni kuweza kuweka matumizi bora ya Faida za kiuchumi na si bahari tu nchi ya Tanzania tumebarikiwa kupata vyanzo vikuu vya maji yakiwemo maziwa na mito ambayo yanaweza kufanya shughuli za bahari na kiuchumi hivyo shughuli ambazo zinatumika kwenye uchumi zinaleta mafanikio katika nchi yetu zinahusisha sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya uchukuzi inawezesha kusafirisha bidhaa kutoka kwenye bidhaa. " Amesema Dkt Gurumo"
Aidha kwenye masuala ya uvuvi zipo kwenye sekta ya uchukuzi. Lakini ni sehemu ya uchumi wa bluu hivyo ili kupata mafanikio kwenye uchumi wa bluu kuna mambo kadhaa. Ikiwemo utayari wa kisiasa. Na kwenye nchi yetu kwa sasa tumeona utashi ambao unafanywa na sekta husika pia tunahitaji rasilimali watu katika kuwekeza zaidi kwenye uchumi huo wa bluu.
Tunahitaji kupata watu wenye uweledi wa kushiriki kwenye kongamano ambalo tunaenda kulifanya hivi karibuni hivyo chuo cha bahari Dar es salaam tumeona ni vyema kuandaa kongamano hilo kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya bahari ikiwemo uvuvi wa baharini na hiki ndio chuo. Pekee katika nchi yetu ambacho kimeweza kupewa Dhamana. Ya kufundisha masomo ya bahari kwa map an a yake.
Hata hivyo Dkt Gurumo aliongeza kuwa Dhumuni ya kongamano hilo la uchumi wa bluu ni kuweza kutoa elimu,na fursa kwa wadau katika kuweza kujadiliana masuala yanayohusus bahari hivyo kupitia kongamano hilo la uchumi wa bluu unaenda kukua zaidi kwani ni mataifa mbalimbali yanakuja nchini ili kuweza kushirikiana na chuo chetu ili uchumi wetu wa bluu uendelee kukua.
Natoa wito kwa sekta mbalimbali kutoka nchini waweze kushiriki kwenye kongamano hilo ikiwemo taasisi binafsi,za serikali na wizara ya uchukuzi na sekta ya elimu kwani ni vyema zaidi sekta ya elimu iweze kushiriki kwenye kongamano hilo la uchumi wa bluu ambalo litakua Lima mchango mkubwa kwenye nchi yetu ya Tanzania pia niweze kumpongeza Rais Dkt samia suluhu kwa kuweza kushirikiana kwa dhati na chuo chetu katika kukuza uchumi wetu wa bluu nchini
0 Comments