Na Sheila Ahmadi
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhandisi Hamad Massauni amezitaka Jumuiya za Kiraia kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na maadili, uwazi, na uwajibikaji kuhakikisha wanachangia katika maendeleo ya jamii bila kuhatarisha ulinzi na usalama wa nchi au kusababisha mmonyoko wa maadili.
Akizungumza Mara baada ya uzinduzi huo wa kampeni za usajili wa jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa Taifa jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni amesema kuwa ni vyema zaidi kuuwekeza kwenye taifa letu huku ikiwa na kauli mbiu isemayo ‘Usajili wa Jumuiya kwa maendeleo na ustawi wa taifa letu’.
“ hivi karibuni kumeibuka wimbi la kutumia Jumuiya za Kiraia katika kufanya vitendo vinavyo hatarisha amani na Usalama wa Nchi yetu ambapo kuna baadhi ya Jumuiya zinatumika katika kusaidia makundi yenye dhima ya kigaidi, kusambaza propaganda za uchochezi, kuwasilisha agenda za kigeni au wafadhili wa nje ambazo zinaweza kuhatarisha maslahi ya Taifa ikiwemo mmonyoko wa maadili,” amesema. Mhandisi masauni.
Aidha kuna baadhi ya changamoto ya uanzishwaji holela na utitiri wa nyumba za ibada katika maeneo mbalimbali nchini na baadhi ya Jumuiya za dini hususan makanisa na misikiti imebainika kujengwa katikati ya makazi ya watu, kuna mrundikano wa taasisi nyingi kwenye eneo dogo na baadhi ya taasisi kutumia sauti za juu na hivyo kusababisha adha na usumbufu katika jamii,” amesema.
Hata hivyo , amesema baadhi ya Jumuiya za Kiraia zimeripotiwa kujihusisha au kutumika katika kufanikisha kutendeka kwa makosa ya jinai na vitendo vingine vyenye madhara kwa jamii.
Miongoni mwa makosa hayo ni utakatishaji wa fedha haramu, ugaidi na ufadhili wa shughuli za kigaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara haramu ya silaha na uwepo wa Jumuiya za Kidini zinazotoa mafundisho potofu na hatarishi kwa usalama wa raia.
Nitoe wito kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuwezesha ustawi wa jamii katika Mikoa yao ni kutambua kuwa wanao wajibu mkubwa wa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kuondoa changamoto hizo katika jamii.
“Madhara yatokanayo na kuchelewa kutoa ufumbuzi wa changamoto nilizozitaja hapo juu pamoja na udhaifu wa mifumo ya Fedha katika taasisi hizo, umepelekea Taasisi ya Kimataifa ya Financial Action Task Force (FATF) ambayo ilianzishwa na Baraza ka usalama la umoja wa mataifa, kutoa ripoti ambayo inaonesha kuwa Nchi yetu haina mifumo mizuri ya usimamizi na ufuatiliaji wa mienendo wa jumuiya za kiraia zikiwemo taasisi na madhehebu ya dini,”amesema.
Tunaweka mazingira Wezeshi katika kutengeneza mazingira rafiki ya taasisi hizo kutumika au kuwa katika hatari ya kutumika katika utakatishaji wa fedha haramu au kufadhili masuala ya ugaidi na hali hiyo imesababisha Tanzania kuwekwa katika kundi la nchi zinazohitaji ufuatiliaji wa karibu hivyo lazimaa kushirikiana kuondoa changamoto hizo.
Kwenye nchi yetu tumewekwa katika kundi hilo, vyombo vya Kimataifa na Wadau mbalimbali wa Kimataifa wamekuwa wakipewa tahadhari kuhusu udhaifu wa kusimamia Jumuiya hizi ambao unaweza kutumika katika masuala utakatishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.
Naye Msajili wa Jumuia za Kiraia Nchini,Emmanuel Kihampa amesema hadi kufikia Januari mwaka huu kuna jumla taasisi za kiraia 10,690
Wizara ya mambo ya ndani kupitia ofisi ya Msajili wa Jumuiya imekuwa iliendelea na uhakiki na uhishaji wa vyeti lengo likiwa kutambua jumuiya ambazo zipo hai na nyingine ambazo hazipo tena.



0 Comments