Na Sheila Ahmadi
Kampuni ya Dowei Care Technology ambao ni wazalishaji wa Taulo za kike na za watoto (SOFTCARE) kesho wanatarajia kutoa msaada wa bidhaa zao katika hospital ya Taifa ya Muhimbuli katika kitengo cha huduma za mama mtoto lengo likiwa kuendelea kumsaidia mwanamke kujisitiri pindi anapokuwa kwenye siku zake za hedhi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Zarina Hasasni. Zari. The boss lady mara baada ya kusaini mkataba mpya na balozi wa bidhaa hizo ambae ni mfanyabiashara maarufu nchini , Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Victor Zhang amesema wamekuwa wakipata matokeo chanya na yenye tija kutokana na uwepo wa boalozi huyu.
kutokana na kampuni hii tumekuwa tukirudisha faida kwa jamii kwa kushiriki kampeni nyingi za kitaifa ikiwa ni pamoja na ugawaji wa taluo za kike kwa mabint wa shule za msingi na Sekondari.
" tukipata matokeo chanya kwa kumtumia huyu balozi wetu lakini pia kutokana na mtokeo hayo tumekuwa na utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii tunawapunguzia mzingo mabint kwa kukosa taulo za hizo jambo ambalo linawasababishia kukosa masoma pindi wanapokuwa kwenye hedhi zao"amesema Zhang.
Aidha ameongeza kuwa, kampuni hiyo kufanya kazi na balozi huyo amesema wameamua kuendelea na kufanyakazi na Zari kwa maana ameweza kuleta matokeo chanya kwa kampuni yao kwani wamezidi kupata faida.
Naye , Zarina Hassan ambae ni balozi ya bidhaa hizo amesema kampuni hiyo ina kila sababu ya kumuongezea mkataba kwani kupitia yeue kampuni hiyo imekua ikifanga vizuri kwenye soko kutokana na umaarufu wake.
Sambamba na hayo ameishukuru kampuni hiyo ya Dowei kwa kumpa mkataba mwingine tena mnonno huku akiahidi kuendelea kuwasaidia wanawake na watoto wanaoshindwa kupata huduma ya taulo hizo kutokana na kuwepo kwenye mazingira ambayo sio wezeshi


0 Comments