SKECHERS YALETA VIATU VINAVYOZUIA MAUMIVU KWENYE MIGUU.

 

Na Sheila Ahmadi

Skechers yaleta  viatu vinazozuia maumivu kwrnye miguu ili kwenda  kuhakikisha kuwa wateja wake wanavaa viatu Bora kwa afya Skechers imekuja na viatu ambavyo vimetengenezwa kwa teknolojia ya Hali ya juu (viatu tiba) ambayo havisababishi maumivu Wala malengelenge kwa watumiaji.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam Meneja masoko wa Skechers Tanzania, Micky Decha amesema kampuni hiyo imeamua kuja na viatu hivyo ili Kupunguza magonjwa ya miguu yanayotokana na viatu kwa watanzania.


Aidha Dkt Jamil Suleiman kutoka hospitali ya Tiba Healthcare amesema kwa muda mrefu kumekuwa na watu wanaogua maumivu ya mgongo na miguu ambao wengi huugua kutokana na viatu wanavyovaa.


Ameongeza kuwa kupitia viatu hivyo ambavyo vimeletwa na kampuni ya Skechers Hapa nchini vimewasaidia watanzania wengi ikiwemo wagonjwa ambao yeye amekuwa pia akiwatibu.


Katika hatua nyingine  amesema Viatu hivyo vina uwezo wa kuvaliwa kwa muda mrefu bila maumivu yoyote ya miguu kwani vimetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu.

Post a Comment

0 Comments