Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah, leo Juni 20, 2026, wameshuhudia utiaji saini wa hati nne za makubaliano ya ushirikiano katika sekta za biashara, maendeleo ya biashara ndogo na za kati, ulinzi pamoja na ushirikiano wa Miji.
Miongoni mwa makubaliano hayo ni yale ya ushirikiano kati ya Manispaa ya Mji wa Zanzibar na Manispaa ya Swakopmund Nchini Namibia, yaliyosainiwa na Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar, Mohamed Ibarim Raza maarufu Razalee (MR SEMATENAA 🇹🇿 🌍).
Hafla hiyo imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam kabla ya viongozi hao wawili kuzungumza na Waandishi wa Habari.




0 Comments