TUZO ZA MUZIKI TANZANIA (TMA) IMEJIPANGA VYEMA KUBADILISHA TASNIA YA TUZO YA MUZIKI KIMATAIFA 2024.

 

Na Sheila  Ahmadi

Tuzo  za Muziki Tanzania (TMA)  zimejipanga vyema kwenda kubadilisha  tasnia ya tuzo za muziki kutoka Tanzania na Afrika kwa namna ambavyo haijawahi kufanyika  kupitia kwenye tuzo ambazo zinaenda kutolewa kwa wasanii mbalimbali na wazalishaji wa muziki Nchini tuzo hizo zikiwemo wimbo  bora ya mwaka ,  Mwanamuziki bora wa kiume na kike,mwanamuziki chipukizi wa Mwaka,wimbo bora wa ushirikiano wa Mwaka mwimbaji bora wa singeli na tuzo mbalimbali ambazo zimeandaliwa na TMA.


Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Katibu mtendaji wa baraza la Sana'a la Taifa   Basata  Dkt  Kedmon  mapana mara baada ya kuzungumza na wanahabari ambapo Amesema kuwa  Tuzo hizo za TMA kwa mwaka huu unafanywa kwa weledi mkubwa huku kamati husika ikizingatia maoni na ushauri  wa wadau wa muziki nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla ambapo wanaoenda kuwania tuzo hizi ni wasanii ambao wanaojishuhulisha  na sanaa ya muziki waimbaji na wachezaji,na watayarishaji ambao wametoa nyimbo Kati ya January moja na disemba 31 2023.


"DKt  Mapana Amesema kamati imeona vyema kuweza kubadili namna ya tuzo zinazofanyika na kuweka ubunifu wa kimataifa huku kamati ikitarajia kuandaa usiku wa "TMA prelude"  ambao utafanyika tarehe 14 mwezi juni mwaka huu tukio hilo litakuwa ni la A wali kabla ya tuzo lengo ni Kuweza kuheshimisha Mashujaa wa tasnia hii ya Muziki "Amesema Dkt Mapana.


Aidha  Tukio hilo la kihistoria linaenda kuhudhuriwa na usiku wa sherehe kubwa na hadhira mbalimbali kutoka Tanzania na kimataifa ili kwenda kuendeleza sanaa ya muziki  ambapo inaenda kuwa maalumu kwa ajili ya kusherekea Mafanikio ya washindi wa tuzo hizi za TMA 2024.


Kwa upande wake Mwenyekiti  Wa  baraza la sanaa Taifa Basata  Bw David minja ametoa wito kwa umma kuhusu makubaliano yaliyofanyika na kampuni kubwa duniani " Paramount  Afrika". Ambayo inamiliki na kuendesha vituo vya runinga ambavyo vinafahamika kama BET na MTV Base ambapo kampuni hii inaenda kushiriki hafla ya kutangaza matangazo yote mubashara.


Kamati inapenda kuwaomba wapenda burudani wote nchini Tanzania na duniani wasikose tukio hili la kihistoria linaloenda kuinua muziki wa kintazania kwenye viwango vipya katika nyanja mbalimbali.


"Tunafuraha kubwa kushiriki na kutangaza matukio yote ya usiku huo wa TMA 2024   kwani kunaimarisha zaidi maono yetu na kuendelea kusherehekea, kukuza,na kuonyesha nguvu ya muziki, ubunifu na utamaduni wa pop na kwenda kuhamasisha vijana wa kiafrika kuingia kwenye sekta hiyo ya muziki " Amesema Monde Twala  ambae ni makamu wa Rais mwandamizi wa paramount Afrika na BET International.

Post a Comment

0 Comments