Na Sheila Ahmadi.
Shirika la Reli Nchini Tanzania (TRC) limeanza rasmi na majaribio ya treni ya umeme kutoka Dare salaam hadi mkoani dodoma ambapo kwenye uzinduzi huo viongozi mbalimbali wa dini zote kutoka madhehebu tofauti na viongozi wa serikali na wananchi wameweza kushiriki katika uzinduzi huo huku waziri mkuu Mh Kassimu majaliwa amesema kuwa kupitia uzinduzi huu ni mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa jijini Dar es salaam mara baada ya kuzungumza na viongozi wa dini zote,viongozi wa serikali ambapo amesema kuwa Dkt samia anatambua mchango mkubwa wa viongozi wetu wa dini zote kupitia mambo mbalimbali hivyo kwenye safari hii ya uzinduzi inaenda kuwa historia ya kwanza ya uzinduzi kusafiri na viongozi hao wa dini kutoka mkoani Dar es salam mpaka Dodoma.
Kuelekea miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Viongozi hao hao wa dini watafanya ibada kuu ya kuliombea Taifa katika viwanja vya Jamhuri jijini dodoma dhumuni ni kuweza kuendeleza mipango mikakati ya Maendeleo kupitia kwenye ushirikiano wa serikali na viongozi hao wa dini hivyo wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu. "Amesema Waziri majaliwa"
Aidha Waziri majaliwa ameongeza kuwa serikali imeweza kuboresha miundombinu nchini kote hususani Miundombinu ya barabara huku viwanja vya ndege vikiendelea kujengwa mikoa yote na miradi mbalimbali ikiwemo bwawa la mwalimu nyerere,bwawa la busisi na mradi huu wa SGR ambao unaenda kurahisisha usafiri wa haraka kwa watumiaji wa treni hiyo.
Kwa upande wake Naibu waziri wa uchukuzi David Kihenzile Amesema kuwa sisi kama wizara tutahakikisha kutoa huduma hizo kwa wakati hivyo miongoni mwa. Majaribio ya vitendea kazi. Vipo ambavyo ni mabehewa, Miundombinu ya reli kutoka stesheni ya Dar es salam ,morogoro na Dodoma hivyo wananchi wetu wajiandae mwezi julai kupata huduma ya SGR na Huku tukiendelea na ujenzi wa bandari ya kubeba makaa ya mawe kutoka mkoa wa Mtwara na Ruvuma pia na uboreshaji wa reli ya makutupora na tabora.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la reli Tanzania (TRC) Masanja kadogosa ameongeza kuwa. Katika maadhimisho ya Tanganyika na Zanzibar ambao ulifanya kuwa Tanzania kuwa na mafanikio makubwa chini ya uongozi wa Dkt samia suluhu hasani kuwa na ujenzi wa reli ya kisasa SGR inayotekelezwa kwa awamu mbili. Ikiwemo Treni ya kutoka Mwanza Dar es salam, pili ni Tabora -Kigoma.
"Pamoja na uendeshaji wa miundombinu hiyo ya treni Shirika la Reli Tanzania TRC
Linaendelea na mradi huu wa SGR ambao ni miongoni mwa Mradi mkubwa nchini Tanzania. Wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 10 .0 ikiwa na Sawa na thamani ya Trioni 23 .3 za kitanzania Hivyo ujenzi huo wa awamu ya kwanza kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro kimeisha na kipande cha pili kimefiki aslimia 96.6.
Aidha Kadogosa amesema bado tunaendelea kufanya majaribio ya treni hizo katika kiwango cha kimataifa kutoka Dar es salaam hadi Dodoma ikiwa ni maandalizi ya treni ya SGR ifikapo mwezi julay Mwaka huu safari zitaanza rasmi kutokana na Agizo la Mh Rais Dkt samia suluhu hasani hivyo Kabula ya kuanza safari sisi kama shirika tumeona vyema kufanya majaribio na viongozi wa dini zote na viongozi wa serikali. " Amesema Mkurugenzi Kadogosa".
Katika hatua nyingine Mchungaji wa Kanisa la kiinjili Kiluteri Tanzania Dayosisi Mashariki na pwani Dar es salam Gorge Fupe amesema kuwa sisi kama viongozi wa dini tunaishukuru serikali kwa kuweza kushiriki uzinduzi huu wa treni ya umeme. Kwani haijawahi kutokea. Kwa viongozi wa dini kupewa. Nafasi ya kuja kuzindua treni hii hivyo tumepewa heshima kubwa kama viongozi wa dini kwani treni hii ni nzuri na ya kisasa ambayo wanaenda kutumia abiria siku za hivi karibuni.
Pia mwenyekiti Taifa wa jumuiya ya maridhiano na Amani Tanzania shekhe Dkt Alhadi Mussa Salumu ameongeza kuwa serikali yetu ya awamu ya sita inafanya mambo makubwa ya kimaendeleo kwani treni hii ni ya kisasa ambayo wananchi wanaenda kupata huduma hiyo na viongozi mbalimbali tumeweza kushiriki kwenye uzinduzi huu na kufanya ibada maalumu ya kuliombea taifa hivyo nitoe wito kwa wantanzania tuweze kushirikiana katika kuleta maendeleo ya nchi yetu




0 Comments