VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMESHIRIKI DUA YA KULIOMBEA TAIFA MKOANI DODOMA

  


Na Sheila  Ahmadi

Viongozi. Wa dini nchini  wameshiriki. dua ya kuliombea Taifa  mkoani dodoma  Huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Philip Mpango amewataka Wananchi na Viongozi mbalimbali  waendelee kudumisha amani iliopo katika Taifa la Tanzania ili Muungano uliopo uweze kudumu na kuyaishi maono ya Waasisi katika kudumisha amani na Mshkamano hapa Nchini.


" DKt  Mpango ameyasema hayo katika Siku ya Maombi na Dua ya kuliombea Taifa mwaka huu iliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma ambapo amesema Muungano huo imekuwa ukiimarika siku hadi siku hivyo wamekuwa mstari wa mbele kwenye kutatua changamoto pindi zitakazojitokeza.


Hivyo Dkt. Mpango  amesema Muungano umezingatia misingi ya Umoja na Mshkamano hapa Nchini ambapo imeweza kuleta faida mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Taifa kuendeleza kukua licha ya changamoto zilizojitokeza mwaka 2020. "Amesema Dkt Mpango "


Kwa upande wake Makamu  wa Rais wa pili kutoka  Zanzibar Mohammed Abdullah amesema changamoto zinazoukabili Muungano zinaendelea kutatuliwa Kwa Kasi kubwa katika kipindi Cha awamu ya sita chini ya Usinamizi wa Rais  Dr Samia Suluhu Hassani Kwa kushirikina na awamu ya nane Visiwani humo.


Naye   waziri. Wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera bunge na uratibu  Jenesta Mhagama amewashukuru viongozi wa dini kwa kuweza kushiriki  kwenye Dua  maalumu  ya kuliombea Taifa la Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikwemo mradi huu .


Aidha  Waziri  mhagama  Amesema kuwa katika kuleta maendeleo nchini imani inatakiwa kwa kiasi kikubwa hivyo  Rais wetu Dkt samia anatambua mchango wa viongozi wa dini  zote na tunatambua kitendo hichi ni kizuri kwa nchi yetu kwani kitasaidia mambo mbalimbali  ya kimaendeleo kukua zaidi ikiwemo miundombinu. "Amesema waziri .


Sanjari na hayo  Mkurugenzi  mtendaji wa shirika la reli  Tanzania TRC   Masanja kadogosa  amesema kuwa kwa  sasa bado tuko kwenye majaribio. Ambayo kuna mashariti huwezi. Kwenda mwendo haraka  mita sitini hivyo watu ambao wana mashaka  na treni hiyo ya masaa manne kutoka dar es salaam mpaka Dodoma " Amesema mkurugenzi kadogosa".


"Kwa  sasa  tuna vipande sita  ambapo tunaendelea. Na ujenzi hivyo miezi hii miwili ambayo inakuja unaenda kukamilika hivi karibuni na majaribio haya ambayo tunafanya ni kwa agizo la Rais Dkt  Samia suluhu hasani  anatekeleza miradi ya Maendeleo kwa ajili ya kujenga Nchi yetu


"Hata hivyo  Kiongozi wa dini kutoka kanisa la inuka uangaze  Boniface. mwamposa Amesema kuwa lengo la dua hii ni kuweza kuungana katika kujenga uhusiano nzuri baina yetu ya viongozi wa dini na serikali  kwa ujumla ili tuweze kuliombea taifa letu liwe salama.


Serikali yetu  ya awamu wa sita inafanya mambo mbalimbali  hususani kwenye kujenga miundombinu,Shule,na uboreshaji wa elimu sisi kama viongozi wa dini tunatambua mchngo mkubwa wa serikali yetu na tuna imani na viongozi wetu wote ambao wanaingoza nchi

Post a Comment

0 Comments