Na Sheila Ahmadi
Benki ya maendeleo. ya kilimo (TADB) imetoa mafunzo ya mikopo kwa wataalamu wa kilimo nchini ikiwa na lengo Mahususi la kuweza kuhudumia watu mbalimbali Katika huduma hizo za kilimo huku washiriki kutoka Burundi wameweza kushiriki Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Benki ya kilimo kwa kushirikiana na Benki mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) Dkt Kanaely Nnko amesema kuwa Dhumuni la kutoa mafunzo hayo ni kuweza kwenda kutoa mikopo kwenye sekta nzima ya kilimo kwani tumekuja na wahitimu Takribani 52. Kutoka kwenye Benki ya ushirika 20 ambazo zimeshiriki mafunzo haya.
Dkt Nnko Amesema ni fursa kupata washiriki kutoka nchi Jirani huku Benki ya
BOT Academy. Ambapo wameendesha mafunzo haya na chuo Kikuu cha kilimo SUA Sokoine university of Agriculture, Chuo kikuu cha SAUTI St Augustine University ambao wamekuwa washiriki wetu wazuri tangu Mafunzo yameanza mpaka kufikia siku ya mwisho na kuweza kuhakikisha wahitimu wetu wa kwanza wamehitimu na kupata mafunzo "Amesema Dkt Nnko"
"Tumeamua kutoa mafunzo haya mikoani kote kutokana na wakulima waweze kupata uelewa kuhusu kilimo kimekuwa kikiendesha Mafunzo kama haya hivyo mpaka sasa mfuko wetu wa Garantii umeweza Kudhamini mikopo 270 na mikopo hiyo imetolewa na Benki la shirika hilo. Na walengwa wa kilimo. Wa moja kwa moja .tumeweza kuwafikia takribani elfu 24.
Kwa upande wake Makamu mkuu wa chuo kutoka chuo cha Benki ya Tanzania mkoani Mwanza Ephurem masanguti Amesema sisi ni sehemu ya Benki kuu tukiwa na majukumu makubwa ya kuweza kuelimisha Umma. Ikiwa na pamoja na mabenki. ya Fedha pamoja na wafanyakazi wa Benki kuu na Taaluma mbalimbali. Katika kutimiza majukumu yetu Benki kuu ya Tanzania BOT inaelimisha umma na kuchangia dira .
Aidha sisi kama Benki kuu tulipewa majukumu na Benki ya Maendeleo ya kilimo TARB ya kutengeneza programu kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo hususani imeenda kulenga kwenye uelimishaji wa Mabenki na maafisa mikopo ambao wanasimamia Benki ya kilimo katika kuweza kutoa mikopo hiyo" Amesema Makamu masanguti".
Naye Afisa mahusiano Mollen Charles kutoka benki ya Absa Amesema kuwa Tumepata mafunzo kwa wiki mbili ya kilimo ambapo tulikuwa na mtazamo kuhudu kuwakopesha mikopo wakulima wa chini kwani wanachangia katika uzalishaji wa chakula.



0 Comments