Na Sheila Ahmadi
Chama cha wafanyakazi wa Majumbani Chodawu imeitaka serikali kutoa mikataba ya namba 189 ambayo inaenda kutetea haki za wafanyakazi hao kupitia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika Jijini Dar es salam ikiwa na kauli mbiu isemayo kuwa Nyongeza ya mishahara ni misingi ya mafao bora na kinga Dhidi ya hali ngumu ya maisha.
Akizungumza Kwenye Maadhimisho hayo jijini Dar es salaam Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Albert Chalamila amesema kuwa. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt samia suluhu hasani anaendelea kufanya maboresho katika Wizara mbalimbali ikiwemo Afya,elimu na nyinginezo hivyo mishahara ya wafanyakazi ikipanda inakuwa suluhu katika kupunguza hali ngumu ya maisha katika nchi yetu ya Tanzania na kuongeza vikokotoo kwa wafanyakazi kwani Rais wetu ni msikivu kwa wananchi wake.
Waajiri wote nchini wanatakiwa kufanya ukaguzi mara kwa Mara wakiwemo.osha kuhakikisha wanatoa huduma kwa haki hivyo nitoe rai kwa wafanyakazi wote kutoa Uhuru wa kazi kwa watu ambao wana hali ya nchini hivyo suala la ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi wote linafanyiwa kazi na tunatambua kua Dar es salaam kuna mvua ambazo ziliharibu miundombinu hivyo wizara husika inatakiwa ifanyiwe kazi katika kurudisha miundombinu ikiwa salama "Amesema RC Chalamila .
Naye katibu Kutoka chama cha wafanyakazi wa Majumbani Chodawu. Wagala shungu amesema kuwa wafanyakazi wa Majumbani wameweza kushiriki katika maadhimisho haya ya wafanyakazi kwani wafanyakazi hawa ni kama wafanyakazi wengine kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi.
Vilevile mfanyakazi wa Majumbani Maua issa amesema kuwa kuna changamoto ambazo wanakutananzo kutoka kwa waajiri wao ikiwemo kutopata Uhuru wa mawasiliano na familia zao hivyo sisi kama wafanyakazi tunamuomba Mh Rais Dkt Samia suluhu hasani aweze kutoa mkataba namba 189. Ili uweze kutetea haki zetu za wafanyakazi pindi tuwapo kazini.
Aidha amesema kuwa tunafanya kazi masa 24 ya kazi na kukosa mda wa kupata chakula na kutopewa mishahara kwa wakati,na kukosa likizo za uzazi kwani mda mwingine tunafanya kazi za waajiri pia serikali yetu ituangalie kwa jicho la pili katika kuweza kutatua changamoto hizi ili tuweze kujikidhi majukumu yetu ya familia katika kusomesha watoto wetu shuleni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Majumbani Zahini Athumani ameongeza kuwa kwa siku hii ya Leo tumefurahi kuungana na wafanyakazi wezetu katika kuadhimisha siku ya Wafanyakazi duniani pia tumefurahi kuweza kutambulika Katika siku hii ya muhimu ya leo tukiwa nankauli mbiu yetu isemayo kuwa "Wafanyakazi wa Majumbani ni sawa na wafanyakazi wengine "
"Sisi kama wafanyakazi wa Majumbani tuna mchango mkubwa hapa nchini Hivyo tulikua tunaomba serikali yetu ya awamu ya sita iweze kuridhia ombi letu la mkataba Maalumu wa 189 ili tuweze kupata mikataba sahihi kutoka kwa waajiri wetu nchini. Kutokana mkataba huo kuwa na miongozo ya kazi ambayo itawezesha kutimiza majukumu yetu kwa uhakika na uadilifu.


1 Comments
Nice
ReplyDelete