Na Sheila Ahmadi
Mabalozi ambao wanawakilisha nchi zao za Afrika hapa nchini wanatarajia kushiriki katika Mbio za Afrika Day Marathon zitakazofanyika Mei 18, Mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza. jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mashariki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Alli Bujiku amesema kuwa mabalozi hao wanaenda kushiriki Afrika day marathon.
Aidha Balozi Bujiku amesema kuwa mbio hizo ni kama sehemu ya kukumbuka kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika (OAU) Mei 25, 1963, Adisababa nchini Ethiopia uliokuwa na lengo la kuzikomboa nchi ambazo hazikuwa huru kwa wakati huo.
Hivyo mbio hizo zitakuwa za kilometa 5 na 15 na zitahusisha mabalozi na baadhi ya maofisa wa kibalozi na Watanzania kwa ujumla na kwamba wanariadha wa Kitanzania ambao wameweka alama kimataifa, Juma Ikangaa, Alphonce Simbu, Filberty Bayi na wengineo watarajia kuwemo katika mbio hizo.
"Ameongeza kuwa zaidi ya mbio hizo maalumu ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 61 ya kuanzishwa OAU mwaka 1963 na mwaka 2002 kubadilishwa jina na kuitwa (AU) baada ya nchi zote za Afrika kuwa huru na sasa wakiwa wanaangalia mafanikio na kupanga mikakati ya kusonga mbele na kujiletea mafanikio katika nyanja mbalimbali.
“Nchi nyingi za Afrika zinaadhimisha siku hiyo Mei, 25 kila mwaka, kwa Tanzania tunaadhimisha Mei 20, kutokana na Mei 25, 2024 kutakuwa na ugeni wa Baraza la Amani na Usalama,” amesema. Bujiku
Vilevile ameongeza kuwa baada ya mbio hizo, watapeleka misaada katika shule zenye wahitaji maalumu nne, mbili zikiwa za Shule za Msingi na mbili za Sekondari ambazo ni Jangwani, Pungu, Uhuru Mchanganyiko na Jeshi la Wakovu.


0 Comments