BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB ) YAANZA KUTOA MIKOPO KWA MWAKA 2024/ 2025

 

Na  Sheila  Ahmadi

Bodi  ya  Mikopo  ya  wanafunzi  wa elimu ya juu HESLB  inatarajia kutoa mikopo kwa Wanafunzi 250,000 wa vyuo vya kati na elimu ya juu ili kwenda   kunufaika na mikopo katika mwaka wa masomo 2024/2025 ambapo Sh bilioni 787 zimetengwa.


Aidha Idadi  ya wanafunzi imeongezeka kutoka 224,056 wa mwaka 2023/2024 ambapo watakaonufaika ni wa shahada za awali, stashahada, stashahada ya umahiri katika mafunzo ya sheria kwa vitendo, shahada za umahiri na uzamivu na ruzuku za Samia.


Hayo   yamesemwa  jijini. Dar es saalaam  na Mkurugenzi. Mtendaji  wa HESLB. Dkt  Bill Kiwia ambapo amesema kuwa  uzinduzi wa msimu mpya wa uombaji mikopo    ya Wanafunzi  dirisha la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao litakuwa wazi kwa siku 90 hadi Agosti 31,2024 na kusisitiza kuwa hawataongeza muda.


"Mkurugenzi  Huyo  amesema.kuwa  Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Dk. Bill Kiwia, akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa uombaji mikopo kwa mwaka 2024/2025.


“Kwa uzoefu wetu siku 90 zinatosha kwa kuwa mwombaji akiwa amejiandaa na nyaraka zote muhimu inamchukua muda wa dakika 40 kukamilisha maombi yake kwa njia ya mtandao. Hivyo, tunasisitiza waombaji wa mikopo kuzingatia muda uliotolewa kwa kuwa hatutarajii kuongeza baada ya Agosti 31,” amesema Dkt  Kiwia.


Vilevile. Dkt  kiwia  Ameongeza kwa kusema mwombaji anatakiwa kuwa na akaunti ya benki na kwamba kwa waombaji wenye namba za nida watapaswa kuziweka wakati wa kuomba mkopo na kama mwombaji hana anaweza kuendelea na maombi bila namba hiyo.


Nitoe  wito  kwa wanafunzi wanaoomba mkopo kusoma na kuzingatia maelekezo yaliyomo katika miongozo ya utoaji mikopo na ruzuku ambayo tayari imewekwa kwenye tovuti ya bodi hiyo ikiwa katika lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Post a Comment

0 Comments