TEMEKE KUZINDUA BALOZI ZA WAFANYABIASHARA.


Na Nancy Mawole 


JUMIUIYA ya wafanyabiashara inatarajia kuzindua balozi za wafanyabiashara kwenye mitaa yote ya Temeke.


Hayo yamesemwa leo Februari 22, na Mwenyekiti wa Wafanyabashara wa Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni 

muendelezo wa ziara ya kutembelea maeneo ya biashara jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti huyo amesema lengo la uzinduzi huo ni kuhamasishaji ya kulipa kodi ndogo kwa wingi, kumiliki TIN namba pamoja na leseni pia kufanya makadirio ya kodi na kuyalipa.


“Uzinduzi huo utahusisha wafanyabiashara wa eneo hili pamoja na kuwakilishwa na viongozi mbalimbali wa nchi,” amesema 


Ameahidi kuwa yeye  pamoja na wasaidizi wake ikiwemo Katibu pamoja na sekretariat watahakikisha  wafanyabiashara wote wanalipa kodi kwa maslahi ya kodi.


Amesiitiza ushirikiano serikali pamoja na wafanyabiashara wote katika kuinua wigo wa kodi.” Tax base bado ni ndogo, hivyo wafanyabiashara wote wakiingia kwenye tax base, kwa uwingi wetu tukilipa kodi nyingi dhana yetu ya kupunguza kodi na viwango vya Tax kuwa rate ndogo vitakuwa vimesikika na Serikali.”


Amesema anaamini kuwa Tax base ya Tanzania kuwa juu ukilinganisha na Kenya pamoja na South Afrika.


Naye Riziki Ngaga Katibu wa Wafanyabiashara katika Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa wiki ijayo wanatarajia kutembelea eneo la Tandika.


Amesema lengo la ziara hii ni kutatua changamoto zinazowakumba wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali.


“Sisi tunaamini kwamba ukifanya biashara haupaswi kuwa na matatizo ili biashara iendelee; mfano wenzetu wanaofanya biashara ya magari katika eneo la Temeke walikuwa wanateswa na eneo la kuegeshea magari pale ambapo vyombo hivyo vinatoka bandari vinavyoleta mizigo katika soko la Temeke na kutozwa gharama za kulipwa; hivyo Mkurugenzi ameahidi kuondoa gharama hizo,” amesema


Amesema pia atashughulikia  changamoto ya kukosa eneo kuegesha magari ilikuweza kupakia bidhaa za wafanyabiashara hao.


Amesema pia Mkurugenzi ahaidi kutatua changamoto ya kulipia gharama kwa magari ambayo yamebeba bidhaa zenye uzito wa kuzidi. 


Ameahidi kuendelea kuunganisha wafanyabiashara kwa ajili ya wafanyabiashara kupata huduma kwa serikali na kulipa kodi kwa wakati.

  

Naye Godfrey Mtei, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wilaya ya Kinondoni amewaasa wafanyabiashara kudhuria mikutano hii ikiwa lengo la ziara hii ni kutatua kero za wafanyabiashara hao.









Post a Comment

0 Comments