Na Sheila Ahmadi
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imezindua rasmi kampeni ya fichua ambayo inaenda. Kurejesha mikopo kwa wale ambao walipewa kutoka vyuoni hivyo bodi ya mikopo tunaenda. Kufichua madeni sugu kwa wahusika ambao walipatiwa mikopo hiyo.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HELSB),Dkt Bill Kiwia, ambapo amesema kuwa hali ya urejeshwaji mikopo kwa sasa baadhi ya wanufaika nchini inaridhisha ambapo sasa wanapokea bilioni 12 kwa mwezi toka bilioni 2.5 mwaka 2016.huku ongezeko la urejeshaji huo ukiwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Aidha. Dkt Kiwia, amesema kuwa kampeni ya kuwafichua wanufaika wa mikopo ambao wapo mtaani wasiotaka kurejesha Mikopo huku wana maisha ya kuweza kurejesha kwa wakati tumeanzisha kampeni hii rasmi kwa lengo la kuweza kukusanya mikopo hiyo ili iende kwa vijana ambao wanasoma vyuoni na kutimiza malengo yao.
"Mwaka 2016 tulikuwa tunakusanya bilion 2.5 kwa mwezi,lakini kwa sasa hali ni nzuri tunakusanya Bilioni 16 kwa mwezi toka kwa wanufaika laki mbili wa mikopo hiyo"Amesema Dkt Kiwia.
Hivyo Dkt Kiwia,amesema kwa sasa Tanzania inashika nafasi nzuri Barani Afrika kutokana na hali nzuri ya urejeshwaji mikopo hiyo na sisi kama bodi ya mikopo tumeona vyema kuanzisha kampeni hii katika kukamilisha ndoto za vijana nchini na wenye uhitaji.
Dkt Kiwia,amesema kampeni hiyo ya awamu ya kwanza itadumu Takribani kwa miezi miwili itawapa nafasi wananchi kwa watanzania kuwataja wanufaika ambao wapo mitaani ambao hawataki kurejesha mikopo hiyo.
"Kama unamuona mtu unamjua amenufaika. Kupitia mikopo hiyo unaweza ukataja jina lake,eneo analofanyakazi,chuo alichosoma kwenda kwenye namba 0736665533"Amesema Dkt Kiwia.
Naye. ,Mkurugenzi. Wa urejeshaji na urejeshwaji kutoka bodi ya mikopo CPA George mziray. amesema kuwa katika kampeni hiyo wanatarajia kuwafikia Wanufaika zaidi ya elfu hamsini huku wanatarajia kukusanya zaidi ya bilioni mia mbili nchini.




0 Comments