KONGAMANO LA UCHUMI WA BLUU KUANZA. RASMI JULAY 4_ 5 JIJINI DAR ES ALAAM.

 

Na  Sheila  Ahmadi

Chuo Cha Bahari  Dar es saalam DMI  kwa kushirikiana na Chuo cha bahari kutoka Ghana  wameandaa kongamano la  kitaaluma  ambalo litahusisha washiriki mbalimbali kutoka nchini wakiwemo viongozi wa Taasisi,  taasisi binafsi, taasisi zisizo za kiserikali, huku watu kutoka  Kenya,  Comoro,  Liberia,  Ghana,  Nigeria, Italy, na nyinginezo zitashiriki kwenye kongamano hilo.


Hayo yamesemwa  jijini  Dar es salaam na Mkuu wa chuo cha bahari dar e salaam DMI Dkt  Tumaini. Gurumo amesema kuwa  kongamano hili la uchumi wa bluu ni la tatu  kwani tunaenda kutoa elimu  kwa kushirikiana watu mbalimbali katika kuendeleza uchumi wetu kutoka kwenye vyanzo vya maji vikiwemo bahari, maziwa na mito.


"Uchumi wa bluu unajumuisha bahari ya Hindi kwani   nchi yetu ya Tanzania tumebarikiwa maziwa makubwa likiwemo ziwa Victoria, Tanganyika na ziwa nyasa hivyo tunaona kwenye uchumi wa bluu tunapata faida mbalimbali za mito na kuweza kutambua matumizi yake ikiwemo kutoa vitoweo  kutoka baadhi ya bahari na maziwa nchini kwetu.


Aidha uchumi wa bluu unatupatia usafiri wa majini  kwani baadhii ya vyombo vya maji hutumia  maji katika kuwezesha uvuvi wa bahari na vingine kutumika katika kusafirisha abiria wanaosafiri kwa njia ya maji na kusafirisha mashehena ya vitu kutoka kwenye maji hivyo maji ni uchumi wa nchi katika maendeleo ya nchi yetu " Amesema Dkt Gurumo".


Nitoe   wito kwa watanzania wote nchini katika kushiriki katika kongamano hili tunaloenda kulifanya kwani tutatoa mafunzo na elimu kwa watumiaji wa vyombo vya majini wakiwemo mabaharia kutoka nchini hivyo kila mtu ni mdau wa uchumi wa bluu tunatakiwa kushiriki kwa pamoja ili tuendeleze uchumi wa bluu katika kukuza sekta ya uchumi wetu.


Vilevile  Dkt  Gurumo  ameongeza kuwa. Kongamano hilo litafunguliwa na Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Dotto  biteko  ambapo watalaamu wote kutoka sekta ya bahari,  utalii,  Bandari,  mafuta na gesi , uvuvi watashiriki katika kutoa elimu lengo ikiwa ni kutoa ujuzi kwa watumiaji wa vyanzo vya maji huku kongamano hilo likiwa na kauli mbiu isemayo kuwa "  KUIENDEA  KESHO KUJUMUISHA  UlINZI  NA USALAMA  WA MAJINI  MABADILIKO  YA  TABIA YA NCHI  NA. MAENDELEO  YA TEKNOLOJIA  KWA UKUAJI  WA UCHUMI WA BLUU"

Post a Comment

0 Comments