UVCCM YAFANYA ZIARA TRC, TPA, YAKOSHWA NA UTEKELEZAJI ILANI



Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wakiongoza Mwenyekiti Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) wametembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Shirika la Reli Tanzania na Bandari ya Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo wamefika kituo Cha reli ya kisasa (SGR) cha Dar es salaam na kupokelewa na Mkurugenzi wa shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa.

Ziara hiyo imelenga kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwenye mradi huo na kupata elimu ya namna Shirika la Reli Tanzania (TRC) linajiendesha mara baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Hata hivyo ziara hiyo inahusisha Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Wenyeviti wa Mikoa yote nchini na Makatibu wa UVCCM Mikoa yote.

Post a Comment

0 Comments