VYAMA VYA SIASA VYATAKIWA KUEPUKA MIGOGORO YA KISIASA.

 


Na   Mwandishi. Wetu

Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa kuepukana na migogoro ya kisiasa kwani inapasua vyama na taifa kwa ujumla .


Akizungumza.  jijini Dar es Salaam  Jaji. Francis Mutungi   mara baada ya  kufungua mafunzo ya siku mbili kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini ikiwa lengo ni kujenga mabadiliko ya uendeshaji wa vyama hivyo.


Jaji Mutungi amesema vyama vya siasa ni taasisi ya umma hivyo vinapaswa kusajiliwa na kutenda majukumu yanayotambulika kidemokrasia na kuachana na vurugu ambazo zinasababisha vyama hivyo kuwa na mpasuko.


mafunzo  haya  ambayo. Tunafanya  yataenda kusaidia kuepukana na mambo mbalimbali ikiwemo mogogoro ya ubadhirifu wa chama na kuingia kwenye matumizi mabaya ya fedha za chama hali ambayo imekua ikiripotiwa kwenye taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali CAG"amesema Jaji Mutungi.


Pia.  amevitaka vyama vya siasa kuwa vinara wa kujenga nchi na kwamba Tanzania sio nchi ambayo inapata utawala kwa mabavu bali ni demokrasia iliotukuka.


Naye , Katibu Mkuu wa ACT - Wazalendo amesema kuwa migogoro ya vyama vya siasa inapaswa kutatuliwa kwa njia ya maridhiano .


"Migogoro inapasua vyama ni vyema vyama kutatua mihogoro kwa njia ya maridhiano tunaishukuru ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kutuletea mafunzo haya kuondokana na migogoro kwenye vyama vyetu"amesema Ado.


Kwa  upande. Wake. Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Demokratic Part (DP) Philipo Fumbo ameshukuru kupatiwa mafunzo hayo huku akisema vyama vingi vya upinzani havina ruzuku kutoka serikalini kushindwa kuajiri wahasibu na maafisa ununuzi hali ambayo imekua ikileta migogoro ndani ya vyama kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Post a Comment

0 Comments