PROF .MBARAWA AMEITAKA MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA TPA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO.

 

Na Mwandishi  wetu

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa  ameigiza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha inasimamia kikamilifu ukusanyaji mapato pamoja na miradi inayotekelezwa chini ya mamlaka hiyo, ambayo  serikali imewekeza pesa nyingi kwaajili ya maendeleo ya kiuchumi nchini. 


Waziri Mbarawa ameyasema hayo alipotembelea Bandari  ya Ndumbi pamoja na bandari ya Mbambabay ambayo ipo kwenye hatua za awali za Ujenzi inayotarajiwa kugharimu kiasi cha  Bil 75.84 hadi kukamilika kwake, Mbarawa amesema  serikali ya awamu ya sita imewekeza pesa nyingi kwenye ujenzi wa Bandari nchi hivyo ipo haja kwa TPA kusimamia miradi na makusanyo kikamilifu.


“Mh Rais anaweka hela lakini sasa wenye jukumu la kusisimia mradi ni sisi serikali yaani wizara pamoja na TPA kazi yangu ni kuwambia TPA wasiamamie mradi huu kwa uadilifu mkubwa, TPA tujipange tuhakikishe kwamba Bandarini hasa Dar es Salaam na maeneo mengine hakuna upotevu. Wa fedha  maanake unachelewesha utekeleaji wa miradi yetu” alisema Mbarawa.


Aidha amesema kama mapato yatakusanywa kikamilifu yatasaidia kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya uchukuzi hasa kwenye uendelezaji wa miradi ya bandari pamoja na miundombinu yake.


“ tusimamie mapato yote yanayokusanywa  kwasababu bila mapato kazi zote hizi hatuwezi kuzifanya bahati nzuri kweny bunge lililopita na serikali imetukubalia kutupa wafredge kwaajili ya kuendeleza miundombinu tuendelee kukusanya sana kule tukikusanya wafrege nyingi na matokeo yake kazi nyingi zitaendelea za utekelezaji wa miradi hii ya bandari” 


Katika hatua  nyingine Mbarawa akizungumzia ujenzi wa bandari ya Mbamba bay amesema bandari hiyo  ni muhimu, na itasaidia kufungua shughuli za kiuchumi kwenye maeneo  ambayo yamepakana na ziwa nyasa hasa kweny kurahisisha shughuli za kiabiashara baina ya nchi jirani kama Malawi na maeneo mengine. 


“Kwa vile bandari hii ni muhimu sana kwa uchumi  kwa nchi yetu ya Tanzania na kwa uchumi wa nchi za jirani na  sisi tumejipanga kuhakikisha bandari hii inajengwa kwa muda ambao tumekubaliana” alisema Mbarawa


Kwa upande wake Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amesema bandari ni moyo wa uchumi wa Wilaya ya Nyasa, iwapo serikali itakamilisha na ujezi wa bandari ya Mbamba Bay itakua imesaidia wananchi kwa kiasi kikubwa. 


“Bandari hii ya mbamba bay ni moyo wa uchumi kwa sisi wana nyasa, bandari hii imekua ni tegemeo kubwa kwa wananchi wano ishi maeneo haya, hata biashara zetu za mihogo, kahawa hii ni bahati kubwa ukitegemea sisi tupo jirani na nchi ya malawi”, alisema mhandisi Manyanya.


Naibu Mkurugenzi mkuu Mhandisi Juma Kijavara akizungumzia hali ya mradi wa ujenzi wa Bandari ya Mbamba bay amesema hadi sasa umeshatekelezwa kwa asilimia 6 na bandari hiyo itahusisha ujenzi wa gati, sehemu ya kuhifadhia mizigo ndani na nje, nyumba za kukaa wafanyakazi pamoja na ujenzi wa barabara ya mita 750 itakayounganisha bandari na wilaya ya Mbinga.


“Kwa hii bandari ya Nyasa  kama tunavyojua kuna barabara ya Mbinga kuja hapa Mbamba bay ambayo inakilomota 66 sasa ile barabara haijaunganishwa na bandari yetu ambayo sasa kwenye huu mkataba ambao tumeingia na mkandarasi wetu tuna hizo mita 750 za kuonganisha barabara hiyo na bandari yetu,


 lakini pia pole tunajenga Gati  sehemu za kuhifadhia mizigo za ndani na nje, na pia tuanjenga na yumba za kukaa wafanyakazi,” 


Mradi wa mamba bay unatekelezwa na Mkandarasi Sheman-Ongoing Constraction Company kutoka china pamoja na kampuni ya Anova na unatarajiwa kugharimu takribani Sh. Bil . 75.84 za kitanzania hadi kukamilika kwake na utatekelezwa ndani ya kipindi cha miezi 24.

Post a Comment

0 Comments