Na Sheila Ahmadi
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri mkuu imekabidhi Boti ya Doria (PBSAILFISH) kwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC ) ili kwenda kuweza kukabiliana na vitendo vya kihalifu ikiwemo UVuvi haramu, na madawa ya kulevya katika Bahari na Maziwa Makuu ambao unatekelezwa kikamilifu.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Mara baada ya kupokea Boti hiyo ya Doria Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu DKt Jim Yonazi Amesema kuwa lengo La kukabidhi boti hii ni kuweza kukabiliana na vitendo haramu kwenye Maziwa makuu na bahari nchini zikiwemo Uvuvi,madawa ya kulevya, ambapo Doria hizo ni Mwendelezo wa juhudi za kiserikali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na biashara za magendo.
"Tunatambua kuwa Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mna usimamizi,na uendeshaji nzuri hivyo tumeamua kuja kuwakabidhi ikiwa na pamoja kuweza kuifanyia Matengenezo kinga kwa Wakati hivyo ufanisi utaongezeka katika kazi zenu hususani katika ukaguzi wa meli. Ambazo zinaingia kwenye maji yeti ya ndani.
Aidha Dkt Yonazi Ametoa wito kwa TASAC waendelee kufanya kazi kwa karibu na idara ya Menejimenti ya maafa iliyopo ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa ajili ya kuweza kuratibu progiramu za uokozi wa majanga ya majanga na usalama. na Bahari kwa Ujumla." Alisema Dkt Yonazi.
Naye Naibu katibu Mkuu wizara ya uchukuzi Bw. Ludovicky Nduhiye Amesema kuwa Boti hii kwa shirika letu La Uwakala wa Meli Tanzania TASAC imekuwa chachu katika kutimiza kwa vitendo Dira yetu Ambayo imelenga kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye huduma za uchukuzi na hali ya hewa zenye uhakika, usalama na nafuu.
Kupitia ofisi ya Waziri Mkuu kununua boti hii ya kisasa ni kuweza kuhakikisha TASAC inaweza kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza majukumu ya msingi ya shirika yanayohusu usimamizi wa masuala ya ulinzi, usalama udhibiti wa uchafuzi wa mazingira ya Bahari ambao unatokana na uchafuzi wa Meli.
Vilevile Bw Nduhiye ameongeza kuwa Boti hii itasaidia kwenda. Kuimarisha ulinzi katika Bahari kuu kwani ni ya kisasa na yenye kasi na ina ukubwa ambao itawezesha kufanya ufatiliaji wa har aka na Doria katika maeneo yetu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw mohamed Salum amesema kuwa serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ilk kuweza kuimarisha usalama wa usafiri majini hivyo boti hii inayokwenda kuikabidhi TASAC hivyo boti hii inaenda katika maeneo ya Bahari na Maziwa makuu ikiwa ni kuhitaji mikakati thabiti ya udhibiti wa shughuli hizo.
Aidha serikali imeandaa Mwongozo wa Taifa wa kuweza kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika Bahari na Maziwa makuu wa mwaka 2022 ambaoni mahususi kwa ajili ya kuzuia na kukabiliana na shughuli haramu za baharini.
Pia Bodi ya Menejimenti ya Shirika La Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwa Mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanaendesha shughuli Za majini huku wakiwa katika hali ya usalama.









0 Comments