Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema, tayari ujenzi wa shule 100 za Amali ufundi umeanza katika mikoa mbali mbali nchini.
Ujenzi wa shule hizo za Amali ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Dkt. Samia, kuhakikisha wanafunzi wakimaliza kidato cha nne, watakuwa na uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kuajiri.
Matarajio ya vijana wengi wanaosoma ni wanapomaliza kupata elimu ni kupata ajira na watoto ni wengi sana wote wanasoma kwa matarajio ya kupata ajira.
Prof. Mkenda amesema, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, kuweka msukumo wa mafunzo ya Amali Uhandisi yanayojikita kwenye ujuzi zaidi.
Shule hizo 100 zinazoendelea kujengwa nchini, zitaweka msukomo katika kutoa Elimu ya Michezo, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Ufundi Umeme, Uashi na Useremala.
Ujenzi wa Shule hizo za Amali, utapewa kipaumbele katika maeneo ambayo hayana Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi stadi.

0 Comments