DKT MWIGULU NCHEMBA ASISITIZA WANANCHI KUKOPA KATIKA TAASISI ZA KIFEDHA ZINAZOTAMBULIWA SERIKALI

Dkt Mwigulu Nchemba asisitiza watu kukopa katika Taasisi za fedha  zilizo rasmi,hayo aliyasema tarehe 10 November 2024,katika jukwaa la wizara ya fedha lililofanyika jijiini Dar es salaam,alisema kuwa "Wananchi wapo salama wanapokopa kwenye TAASISI za kifedha na hawako salama wanapoenda kukopa kwenye kausha damu"

"Kama sisi Serikali tunapokuwa na uwangwana tunajadiliana mtu anapolipa"

"Kumekuepo pia watu kufanya njama za makusudi za watu kutokulipa,kuna makundi ambayo yanachukua fedha na wamejipanga kutokulipa mikopo hao wanajiita wanjanja wamjini,na wakiguswa wanaenda mahakamani"

"Tumeongea na wenzetu kuwa masuala yanayohusu uchumi na kodi kushughulikiwa kwa haki na niwapongeze sana wakina mama ni wazuri sana katika kurejesha mikopo"

Na aliongezea kuwa "eneo lolote likichukuliwa kama mama anajua mama atarejesha na mikopo itaenda kwenye sehemu sahihi kuliko wakina baba wakikopa"

"Tuendelee pia katika elimu tunayoitoa kuwa fedha za mikopo inatakiwa ifanye shuguli inayoweza kuzalisha, mfano nchi yetu fedha zinapokopwa zinapelekwa katika miradi ya maendeleo,na inapelekwa katika shughuli ambayo itafanya uzalishaji kama vile Barbara kufua umeme"

Na aliwataka watu wanaotoa mikopo kwenye TAASISI zisizo rasmi kuacha Mara moja ambapo alisema kuwa 

"Tutaendelea kuchukua hatua Kali kwa wale wanaofanya shuguli za kausha damu ili tukomeshe unyonywaji ambao unafanywa.

Vile vile Dkt Mwigulu Nchemba amefanya Uzinduzi wa 

"mikakati ya upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali wa chini na wa wakati."na 

"Kanuni za mikakati za upatikanaji wa mitaji(club funds)"

"Kanuni za miongozo zinazozingatia hati fungani na sheria"


Naye Prof Adolf Nkenda waziri wa Elimu naye aliwataka wadau wa elimu kupitia mtaala mpya wa elimu,ambapo alisema kwamba

"Katika sekta ya elimu tunahitaji wataalam ambao watasukuma gurudumu lisonge mbele"

"Katika kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne, lazima mwanafunzi wasome biashara(ujasiriamali),ili ajue akimaliza ajue anafanya mambo gani"

"Tunataka kijana akimaliza kidato cha nne awe anajua tin number ni nn,na brela ni nini"alisema  Prof Mkenda.








 

Post a Comment

0 Comments