Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu Prof.Daniel Mushi hapo Jana tarehe November 06,2024 alimwakilisha Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia katika mahafali ya 18 ya Duru ya kwanza ya Taasisi ya teknolojia Dar es salaam(DIT) alisema kwamba "Najua elimu mlioipata ni kubwa,ninawaomba tu kuwaasa,mkaitumie kwa manufaa ya jamii,kwa sababu mkitumia maarifa na ujuzi mlionao vibaya mnaweza kuumiza jamii"
Pia aliwazitaka Taasisi za umma,na za binafsi, kuwatumia wahitimu hao wa ufundi sanifu Teknolojia Na uhandisi,ambapo alisema kuwa
"Njooni mshirikiane na wahitimu hawa katika Changamoto zinazotusibu katika Shughuli za kijamii na Kiuchumi"alisema Prof.Mushi.


0 Comments