SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA UCHUKUZI





Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta za  Uchukuzi nchini hususan kwenye eneo la Bandari , Huduma za  Shirika la reli(TRC) na Atcl


Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 19, Desemba, 2024 Jijini Dar es salaam Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Greyson Msigwa amesema kufuatia bandari kuwa lango kuu la uchumi la nchi yetu Serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa kuimarisha bandari zote nchini zikiwemo za bahari na katika maziwa makuu  ili ziweze kuongeza ufanisi na uchumi wa nchi yetu kwa kuhudumia shehena zaidi za ndani na nje


" kuanzia mwezi mei 2024 mpaka Novemba 2024 kiwango cha shehena kilichohudumiwa na bandari zetu zote chini ya TPA ni tani mil 16.5 ambalo ni ongezeko la asilimia 5.2 ukilinganisha na tani mil 15.6 iliyohudumiwa kwa kipindi hicho mwaka 2023, idadi ya makasha 621,584 likiwa ni ongezeko la asilimia 3.29  likilinganishwa na makasha 601,805 mwaka 2023 hii inadhihirisha uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali


Amesema katika kipindi hichohicho kiwango cha shehena kilichohudumiwa na  bandari ya dar es salaam pekee ni tani mil 14.4 sawa na ongezeko la asilimia 5.6 ikilinganishwa na shehena ya tani mil 13.7 mwaka 2023, shehena ya makasha 598,672 ilikinganishwa na makasha 597,613 mwaka 2023 na shehena za nchi jirani tani mil 6.3 sawa na asilimia 19.3  ya ongezeko ukilinganisha na tani mil 5.3 mwaka 2023


Amesema katika kipindi cha miaka 2 iliyopita mageuzi makubwa yamefanyika katika bandari yetu ya dar es salaam ikiwemo kukaribisha kampuni binafsi ya DP Word kuwekeza kwenye bandari ili tuweze kunufaika na fursa zilizopo, ujuzi na mtandao na sekta binafsi ambapo Serikali kupitia TPA ilisaini mikataba mitatu ya uwekezaji na kampuni ya DP Word ya Dubai tarehe 22 Oktoba, 2023 ukihusisha uendelezaji na uendeshaji wa shughuli za bandari katika uhudumiaji wa makasha, mizigo mchanganyiko na shehena ya magari, ili kutoa huduma hizi kwa kuzingatia sheria za nchi yatu kampuni ilifungua kampuni tanzu ya DP Word Dar es salaam iliyokabidhiwa rasmi majukumu tarehe 15 April ,2024


Amesema kama nchi tumeanza kuona matunda kwa kipindi kifupi kutoka mwezi April ,2024  tumepata mafanikio ambapo kwa miaka mitano ilitakiwa iwekezwe zaidi ya Bil 650 lakini kwa miezi mitano tu imeshawekeza shilingi bilioni 214.425  sawa na asilimia 31 ya uwekezaji tulioutarajia, ukarabati wa mitambo iliyokuwepo umefanyika na usanifu, usimikaji wa mifumo ya tehama imefanyika na kazi zimeanza


Amesema manufaa mengine ni Wastani wa muda wa meli kusubiri umepungua kutoka siku 46 mpaka 70  hadi siku 7, baadhi hazisubiri kabisa kama za makasha, za kichele siku 12 ambazo awali zilitumia miezi miwili, mizigo mchanganyiko siku 10 hivyo kupunguza gharama


" Meli zote katika upakuaji wa shehena katika bandari ya dar es salaam baada ya uwekezaji wa DP Word wastani ni siku saba na gharama za uendeshaji wa bandari zimepungua kwa asilimia 2.7 na Serikali kukusanya shilingi bil 325.3 yakiwa ni mapato ya kimkataba na uwekezaji mpya wa zaidi ya Tril 1 kwa makusanyo ya ndani umeanza" amesisitiza  Msigwa


Kuhusu TRC amesema Serikali inaendelea kujenga na kuimarisha  Mtandao wa reli ya kisasa na ya kawaida sambamba na ile ya TAZARA ili kuiunganisha na bandari


Amesema ujenzi wa reli ya SGR unaendelea kutekelezwa kwa awamu ambapo jumla ya thamani ya uwekezaji wa mradi ni Dolla Mil 10.3 sawa na zaidi ya shilingi Tril 23.3 na vipande vingine wakandarasi wako saiti na hakuna mradi wa reli uliokwama


Amesema wakati tunasubiri kumaliza reli yetu yote ya SGR tayari tumeanza kuitumia na matokeo yanaonekana kwa kipande cha DAR-MOR-DOM 


Amesema Serikali inaendelea kuimarisha  miundombinu ya treni,lakini pamoja na hayo yote tumeanza kuona hujuma kwenye miundombinu yetu na kutoa rai ilindwe


Kwa upande wa ATCL Msigwa amesema tunazo ndege za kisasa 15 zikiwemo ndege za abiria 14 na ya mizigo moja

Na shirika letu la ATCL linaendelea kutoa huduma vizuri katika vituo 27,ambavyo vituo 15 ni ndani ya Afrika"


"Pia ATCL inavibali vya usalama kutoka shirika la usalama Duniani ambapo tulipata asilimia 87%"

Na tunaendelea kushirikiana na mashirika mbalimbali Duniani  na ufufuajia wa shirika letu amesema Msigwa"

Post a Comment

0 Comments