ZANZIBAR IMETENGA KIAS CHA BILLION 33.4 KWA VYUO VIKUU.








 Hayo aliyasema Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar,Dk Hussein Ali Mwinyi wakati wa mahafali ya 20 ya  Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar(SUZA)yaliyofanyika hapo jana wilaya ya kati,mkoa wa kusini unguja,katika ukumbi wa Dkt Ali mohamed Shein uliopo Tunguu, Aidha Rais Dkt Mwinyi ni Mkuu wa Chuo hicho(SUZA)ambapo amewatunuku zaidi ya wahitimu 200 ngazi ya vyeti,stashahada,Shahada na Shahada ya uzamili na uzamivu.

Pia Dkt Mwinyi alisema kuwa"Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imetenga  kiasi cha billioni 33.4 kwa ajili ya wanafunzi 8,870."

Vilvile aliongezea kwa kusema"kwa kutambua umuhimu wa elimu,Serikali itaendelea kuchukua kila juhudi kuhakikisha mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa ngazi zote,ili kuwa na wanataaluma wenye weledi na ujuzi,utakaochochea maendeleo na ukuaji wa uchumi"alisema Dkt Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments