Mkuu wa wilaya Ubungo Mhe Hassan Bomboko na kamati ya usalama wilaya hiyo ametembelea na kukagua shule zilizopo wilaya ya Ubungo lengo ikiwa ni kujionea namna shule zilivyo anza kupokea wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa muhula wa masomo wa mwaka 2025
Aidha DC Bomboko ameeleza namna ambavyo serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ilivyo wekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu ya madarasa, vyoo, maabara, nyumba za walimu mabweni na miundombinu mingine hivyo mazingira ya kujifunza ni mazuri na salama.
DC Bomboko amempongeza Mhe. Rais kwa kuwa na dhamira njema na maono makubwa ya kuwekeza fedha zaidi ya Bilioni 29 katika sekta ya elimu pekee ambapo katika fedha hizo shilingi Bilioni 19 ni kwaajiri ya elimu sekondari huku Bilioni 10 ni kwaajiri ya elimu msingi.







0 Comments