SERIKALI YAAHIDI KUFANIKISHA LENGO LA KUWAHUDUMIA WATANZANIA IPASAVYO

 


Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeahidi kuimarisha juhudi za ukusanyaji wa madeni yanayotokana na huduma ya nishati ya umeme, ili kuongeza mapato na ufanisi katika utoaji wa huduma.



Mkurugenzi wa Fedha wa TANESCO CPA. T Jabir Idd, hivi karibuni katika kikao cha Wahasibu wa Mikoa yote nchini kilichofanyika jijini Dodoma amesema

muhimu kuhakikisha tunatekeleza mpango huu kwa ufanisi ili kuongeza mapato na kufanikisha lengo la kuwahudumia Watanzania ipasavyo," ameongeza.


Ameongeza kuwa, Shirika limeazimia kushughulikia changamoto zinazokwamisha ukusanyaji wa madeni ili kuhakikisha watumiaji wa huduma ya umeme wanalipa madeni yao kwa wakati.


“ Kuna changamoto mbalimbali zinazoathiri ukusanyaji wa madeni, lakini kikao hiki ni fursa muhimu kwa Wahasibu wa Mikoa kujadili mikakati ya kuimarisha mfumo wa mapato kwa lengo la kufuatilia madeni kila mwezi na kuhakikisha tunakusanya mapato stahiki kwa ajili ya uendeshaji wa Shirika na utoaji bora wa huduma,” amesema CPA. Jabir.


Aidha, amesisitiza kuwa TANESCO itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato. 


*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments