NA VICTOR MASANGU,RUFIJI
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) leo ameanza ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa wa Pwani na kumpongeza kwa dhati Rais wa awamu sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbi mbali ya kimaendeleo katika sekta mbali mbali.
Hayo ameyabainisha wakati ya ziara yake ya kikazi ambayo ameianza leo rasmi katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa ccm pamoja na jumuiya zake.
Chatanda katika ziara hiyo amebainisha kwamba Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kuwatendea haki wananchi hasa katika Wilaya ya Rufiji katika sekta ya Afya,Elimu,afya,maji miundombinu mbalimbali ya barabara pamoja na uwezeshaji Wananchi kiuchumi ikiwemo fursa za mikopo.
"Serikali ya ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imeweza kuimarisha mifumo madhubuti katika sekta hizo ili kuwaondolea adha wananchi wa Rufiji.
Aidha chatanda katika hatua nyingine amewasihi wananchi wa Rufiji kujitokeza kwa wingi katika kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura litakapowafikia kwa awamu ya pili.
Aidha Mwenyekiti huyo amebainisha kwamba wana ccm na wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Mwezi Oktoba Mwaka Huu kwa kuwa Uchaguzi upo na waachane na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa (UWT) Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha nyingi katika Wilaya ya Rufiji ambazo zimeweza kuleta tija zaidi katika kutekeleza miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Naye Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Mhe. Subira Mgalu amebainisha kuwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo katika kipindi cha miaka minne katika suala la kuwahudumia wananchi na kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.
0 Comments