Hayo aliyasema Mkurugenzi wa malkia Choice FM Ndugu Juhayna Ajmy,Katika Dar malkia Festivals iliyofanyika 30 August 2025 ambapo maadhimisho mwaka mmoja wa Malkiachoicefm yalifanyika jijini Dar es salaam.
Ambapo alisema kuwa" malkiachoicefm "Tulipata baraka kubwa saana ya kusafiri na Mheshimiwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma na akatupa Baraka za kufungua Malkiachoicefm. Hiyo ni Baraka yake kubwa na upendo mkubwa kwake tunashukuru saana"alisema Juhayna Ajmy.
Aidha Vilvile Mkurugenzi aliwashukuru na kuwatia moyo, Malkia na Vijumbe hodari waliofika hapa kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama kwaajili ya kusherekea mwaka mmoja tangu redio ya malkiachoicefm ilipozinduliwa.
Na pia Mgeni Rasmi wa Dar Malkia Festival, aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe Saad Mtambule, pamoja na Rais wa sauti ya wanawake Tanzania Ndugu Maidawaziri.





0 Comments