MKURUGENZI WA MASOKO WA POSTA ATEMBELEA BANDA LA SHIRIKA KWENYE KAHAWA FESTIVAL 2025

 









Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa shirika la posta tanzania, bw. ferdinand kabyemela, akiambatana na meneja wa posta mkoa wa arusha, bw. athumani msilikale, wametembelea banda la shirika la posta tanzania lililopo katika maonesho ya kahawa festival 2025 yanayofanyika mkoani kilimanjaro.


ziara hiyo imefanyika leo tarehe 4 oktoba 2025, ambapo viongozi hao wamepata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo, ikiwemo huduma za usafirishaji wa mazao ya kahawa. sambamba na hilo, wamewahamasisha wakulima na washiriki wa maonesho hayo kutumia huduma za posta katika kusafirisha mazao yao kwa ufanisi, usalama na gharama nafuu.


Post a Comment

0 Comments