Mkuu wa Wilaya ya Rombo Atembelea Banda la Posta Katika Kahawa Festival 2025

 






Moshi, Kilimanjaro – 5 Oktoba 2025


Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Mhe. Raymond Mangwala, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kama Mgeni Rasmi, ametembelea Banda la Shirika la Posta Tanzania katika kilele cha Maonesho ya Kahawa Festival 2025 yanayofanyika mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.


Katika ziara hiyo, Mhe. Mangwala alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Ferdinand Kabyemela, ambaye alimpatia maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo, hususan huduma za usafirishaji kwa wakulima wa kahawa.


Shirika la Posta Tanzania linaendelea kushirikiana na sekta ya kilimo kwa kutoa huduma za usafirishaji nafuu na za uhakika, zenye lengo la kuwasaidia wakulima kufikisha bidhaa zao sokoni kwa urahisi.


Post a Comment

0 Comments