CCM yapongeza hotuba ya Rais Dk Mwinyi kudumisha maridhiano Zbar





Na Mwandishi wetu, Zanzibar 


 Chama cha Mapinduzi  kimepongeza  hotuba  iliotolewa na   Rais wa Zanzibar  na  Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi ,Dk Hussein Ali Mwinyi  yenye nia ya   kuendeleaza  Maridhiano  ya Kisiasa na  Umoja  wa Kitaifa  Zanzibar.


Aidha, CCM kinaona fahari kushuhudia Uchaguzi Mkuu   ukimalizika salama na sasa ni wakati  wa kuleta Maendeleo  na  kuwaunganisha wananchi .


Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar  ,Idara  ya Itikadi  ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto  Khamis mara baada  ya Rais  Dk Mwinyi alipomaliza kulihutubia Baraza  la Wawakilishi  Zanzibar  (BLW) .


Mbeto alisema hotuba   ya Rais  Dk Mwinyi imeweka wazi kusudio la  kuondoa  mivutano na misuguano isio na ulazima katika jamii, kwani masuala hayo aghalab  hukwamisha kasi ya maendeleo .  .


Mbeto alisema kutokana na  uzalendo  wa  Rais ,ameweka bayana msimamo wa  Serikali yake ,alipoahidi   kuyasimamia  maridhiano  na  kulinda Amani, Utulivu  na Umoja   .


Aliwataka  Wanasiasa wa vyama vyote  wawe na   fikra ya kutoendeleza malumbano   ,mivutano na mabishano ambayo kiuhalisia hayana  tija wala faida  baaada ya  uchaguzi kumalizika.


'Kurasa za  Siasa , Uchaguzi  na Ushindani  wa hoja na Sera majukwaani sasa  zimeshafungwa.Lazima  tuwe tayari  kudumisha  Umoja na  kuzitafutia majibu changamoto  za maendeleo ya jamii" Alisema Mbeto. 


Pia Mwenezi  huyo alisema ni zamu ya  wananchi  kuanza kuvifuatilia  vikao vya Baraza la Wawakilishi   kwa  lengo la kuwaona  Wawakilishi wao  wakiihoji ,kuibana na  kuzisimamia   Wizara za Serikali .



Wakati  huo huo, Mbeto alisifu juhudi za Serikali ya Rais Dk  Samia Suluhu  Hassan kwa hatua ya  kuanzisha meza ya  Maridhiano na vyama vya Siasa ili 

kufikia suluhu na upatanishi  . 


Alisema uamuzi wa kufungua pazia la Maridhiano hayo  kati Serikali   na upinzani mara baada ya uchaguzi , azma  ni kuhuisha na kudumisha ustawi wa  Aman ,umoja  ,Haki na  Utawala wa sheria. 


Mbeto ameuita  msimamo  huo wa Rais Dk Samia ni  thabiti  na wenye  hisia na nia ya kuendeleza  uungwana na ustaarabu wa kisiasa nchini  .


Msimamo wa Serikali  yake  ametangazwa na Makamo wa Rais  Dk Emmanuel Nchimbi , aliposhiriki kikao cha  Wakuu wa Nchi kupitia  Kamati ya Maendeleo  Kusini Mwa Afrika  (sadc) 


Katibu  Mwenezi  huyo aliutaja msimamo  huo,  una lengo la kuyatia rutuba   mazingira ili yawe  tulivu na salama,  na kuchochea  shime ya  kudumisha Umoja   kupitia meza ya  mazungumzo .


"CCM kinampongeza Rais Dk Samia kwa msimamo wake  kabambe .Kimsingi amezingatia maoni , ushauri na kusikiliza  sauti za wachache  dhidi  ya  walio wengi ili wote  kuwaweka pamoja " Alisema Mbeto

 

Post a Comment

0 Comments