TLS Wajitolea kutoa msaada wa kisheria ikiwemo kuwawakilisha mahakamani watuhumiwa wote

 .


Waliofikishwa mahakamani tangu tarehe 7 Novemba.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Mawakili ambao ni wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)leo Jijini Dar es Salaam wameelezea mwenendo wa mashauri ya jinai yanayoendelea kufunguliwa kote nchini.

Wakizungumza , kuelezea haki ya msaada wa kisheria kwa watuhumiwa wote hususani ndugu na wazazi wa wanaotuhumiwa katika mashauri hayo wamesema Novemba 7 , 2025 mashauri yanayohusisha kula njama ya kufanya  kosa la jinai, uhaini,uharibifu wa Mali,u yang'anyi wa kutumia silaha,uchomaji wa mali na kufanya maandamano bila vibali yalifunguliwa na Jamhuri.

"Watuhumiwa wengi wa makosa haya ni vijana wenye umri kati ya miaka 19 mpaka 25 baada ya mashauri haya kuanza kufunguliwa tulikaa na kufanya tathimini ambapo tulibaini kuwa watuhumiwa walio wengi  uelewa wao wa kisheria ni mdogo na wengine hawana hata uwezo wa kulipia gharama za mawakili kwa ajili ya kuwawakilisha," amesema mmoja wa mawakili hao William Maduhu.

Maduhu amesema kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 wao mawakili kutoka TLS wameamua kujitolea kutoa msaada wa kisheria ikiwemo kuwawakilisha mahakamani watuhumiwa wote waliofikishwa  mahakamani tangu tarehe 7 Novemba na ambao  wataendelea kufikishwa  mahakamani siku Hadi siku bila malipo na bila masharti yoyote.

TLS imesema idadi ya watuhumiwa waliokuwa wanashikiliwa katika mahabusu mbali mbali kote nchini  inakadiliwa kuwa katika mkoa wa Dar es Salaam pekee zaidi ya watu 400 walikamatwa,Mkoa wa Mwanza watu  zaidi ya 200 walikamatwa, Kilimanjaro takribani watu 312 walikamatwa ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro watuhumiwa 300 wamekwisha achiwa na 12 bado wanashikiliwa.

Wamesema watuhumiwa hao 12 wanashikiliwa huku taratibu za kipelelezi zikiendelea dhidi  yao .

Wameelezea kuwa Mkoa wa Tabora watuhumiwa 5 wanashikiliwa na Jeshi la polisi, Mkoa wa Mbeya watuhumiwa zaidi ya 300 , Njombe watuhumiwa zaidi ya 10 huku Songwe watuhumiwa zaidi ya 200 na Kigoma watuhumiwa zaidi ya 10 walikamatwa. 

Hivyo imeelezwa kuwa Jeshi la Magereza liwape maelekezo kwa ufasaha Wazazi/Ndugu jamaa na Marafiki ambao watoto wao wamekwisha fikishwa mahakamani ili waweze kufika  mahabusu kuwaona  ndugu zao ikiwemo kuwapelekea mavazi na mahitaji mengineyo kwani mahabusu au magerezani ni sehemu ya umma iliyopewa jukumu la kutunza mahabusu na hivyo ni haki ya ndugu kuonana na wapendwa wao.

Imetajwa kuwa kwa wazazi wa Dar es Salaam wawatembelee watoto wao katika gereza la Segerea na walioko katika mikoa mingine wawatembelee katika Magereza yaliyoko Mkoa husika ambapo ndugu wametakiwa  kuwa na vitambulisho wanapotembelea katika Magereza husika.

Kwa upande wake wakili Paulo Kisabo   amesema kuwa wao kama mawakili wanatoa uwakilishi wa kisheria kwa watuhumiwa kote nchini bila ubaguzi.

"Tunatoa wito kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini kutumia Mamlaka yake kisheria kufuta hizo kesi kwani kwa tathmini yetu tunaona mashtaka yaliyofunguliwa hayana msingi wa kisheria,"amesema Wakili Kisabo.

Post a Comment

0 Comments