Kampuni ya Lumac Window imemtambulisha rasmi Kassim Mandonga maarufu kama “Mandela” kuwa balozi wao katika hafla iliyofanyika Aprili 2, 2026 eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo, Mandonga alitumia jukwaa hilo kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa za kampuni hiyo, akizitaja kuwa imara na salama kwa matumizi ya majengo ya kisasa.
“Ukifunga madirisha ya Lumac Window kwenye nyumba yako unakuwa salama. Hii ni ngumi imara—ngumi ya Lumac Window,” alisema Mandonga huku akisisitiza umuhimu wa kutumia bidhaa bora katika ujenzi.
Uongozi wa kampuni hiyo umeeleza kuwa uteuzi wa Mandonga unalenga kuimarisha utangazaji wa bidhaa zao pamoja na kuwafikia wateja wengi zaidi kupitia ushawishi wake kwa jamii.
Aidha, Lumac Window imewataka wananchi wanaojenga kutumia bidhaa zao, ikisisitiza kuwa zina ubora unaokidhi viwango na zinachangia usalama wa majengo.
Kampuni hiyo pia imeeleza kuwa ina mtandao wa mawakala nchi nzima, jambo linalorahisisha upatikanaji wa bidhaa zake kwa wateja wa maeneo mbalimbali.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau wa ujenzi, wafanyabiashara na mashabiki wa Mandonga, huku ikionyesha hatua mpya ya kampuni hiyo katika kupanua soko lake ndani ya Tanzania.


0 Comments