MANGUNGU AMLILIA SHABIKI MAARUFU WA SIMBA EMMANUEL MACHA



NA VICTOR MASANGU, DAR

Maelfu ya wananchi mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini,  taasisi na mashirika binafsi ,mashabiki wa soka na mziki wa dansi pamoja na wananchi mbali mbali .... wamejitokeza kwa wingi   katika makaburi ya Kinonddoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya  kuhudhuria mazishi ya mfanyabiashara maarufu na mshabiki mkubwa  wa klabu ya soka ya Simba Emmanuel  Nderimo almaarufu Macha ambaye alifariki dunia  machi 30 mwaka huu.

Katika mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na chama cha mapinduzi (CCM) yalikubikwa na  vilio na majonzi makubwa ambayo yalipelekea baadhi ya watu kushindwa kujizuia kwa kutokwa na machozi  wakati wa zoezi la kuuga mwili huo.

Moja kati ya viongozi maarufu ambao walihudhulia katika  msiba huo ni Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba Murtaza  Mangungu pamoja ambapo aliambatana na viongozi wengine mbali mbali wa klabu hiyo ambapo amesema marehemu Emmanuel alikuwa  na mchango mkubwa sana  katika klabu hiyo kwani alikuwa mstari wa mbela katika kusaidia mambo mbali mbali

Pia Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya  Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro naye alikuwa ni mmoja wa viongozi wa ulinzi na usalama ambaye naye  alifika kwa ajili ya kutoa heshima zake za mwisho  kwa Marehemu Emmaanuel Nderimo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe,Silvestry  Koka ambaye marehemu ni  shemeji yake hakusita  kumwelezea marehemu jinsi alivyokuwa ni mpambanaji katika mambo mbali nmbali na kwamba alikuwa ni mtu wa kusamehe sana pindi unapomkosea na kwamba alikuwa ni mstari wa mbele katika kutoa ushauri wenye kujenga.

"Kwa kweli mimi nimesimama hapa kwannza kabisa namshukuru mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kutukutanisha hapa katika msiba wa ndugu yetu Emmanuel lakini kitu ambacho nataka kukisema inapaswa tuishi kwa kupendana sana na ndio maana marehemu alikuwa na upendo mkubwa sana  na watu mbali mbali na alikuwa ni mwepesi sana katika suala la kusamehe kwa hivyo inapaswa tujifunze mazuri ambayo ametuachia."amebainisha Mhe. Koka.


Nao baadhi ya  viongozi na mashabiki akiwemo Mama Asha Baraka ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) amesema kwamba ameguswa na kusikitishwa sana na msiba huo mzito kwani marehemu kwa upande wake alikuwa ni moja ya mtu muhimu sana katika kuleta chachu ya maendeleo katika ttimu pamoja na kuweza kusaidia mtu mmoja mmoja kwa hivyo ni pengo kubwa sana ambalo ameliacha.

Pia mwimbaji maarufu wa mziki wa dansi hapa nchini Ally Choki ni moja kati ya wasanii maarufu ambao walihudhulia katika msiba huo hadi kuweza kufika katika makaburi hayo ya Kinondoni kwa lengo la kumpumzisha ndugu yao na rafiki mkubwa wa burudani ya mziki wa dansi hapa nchini katika bendi mbali mbali.

Mazishi hayo ya marehemu Emmanule Nderimo  ambayo  yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam  yameweza kuhudhuliwa na umati wa  maelfu ya watu kutoka sehemu  mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa chama, viongozi wa madhehebu ya  dini, taaasisi wezeshi,wasanii maarufu, pamoja na wananchi ambao wamewza kufika na kumuhifadhi katika nyumba yake ya milele.

                             


Post a Comment

0 Comments