WAANDISHI WATEMBELEA MIRADI YA WRC, WAJIONEA SHUGHULI ZA KIROHO NA KIJAMII

 




Dar es Salaam – Waandishi wa habari wamepata fursa ya kipekee kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika ndani ya World Restoration Church (WRC) chini ya uongozi wa Prophet Suguye, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 19 ya kanisa hilo.

Katika ziara hiyo, waandishi walitembelea maeneo mbalimbali muhimu yanayobeba sura halisi ya huduma za kanisa hilo, likiwemo eneo la maombi maarufu kama “Mlima wa Maombi”, ambalo limekuwa kitovu cha ibada na maombezi kwa waumini wengi kutoka maeneo tofauti. Eneo hilo linaelezwa kuwa na mchango mkubwa katika kukuza maisha ya kiroho ya waumini.

Aidha, waandishi hao walipata nafasi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kinachoendelea kujengwa na kanisa hilo, ambacho kinatarajiwa kutoa huduma muhimu za afya kwa jamii inayozunguka pamoja na waumini. Mradi huo unaonekana kuwa sehemu ya juhudi za kanisa kuchangia ustawi wa jamii zaidi ya huduma za kiroho.

Pia, katika ziara hiyo, walitembelea maeneo ya ufugaji wa wanyama na mifugo mbalimbali yanayosimamiwa na kanisa hilo, hatua inayodhihirisha namna WRC inavyojikita katika kukuza uchumi wa ndani na kujenga mifumo endelevu ya kujitegemea.

Kwa ujumla, ziara hiyo imeonesha kwa upana zaidi namna ambavyo WRC inavyojikita si tu katika huduma za kiroho bali pia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Hatua hiyo inaonekana kuwa sehemu ya maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya miaka 19 ya kanisa hilo, yanayotarajiwa kuwa na mvuto mkubwa kwa waumini na wadau mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments