Dar es Salaam, 24 Oktoba 2026
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, leo tarehe 24 Oktoba 2026, ameshiriki ibada ya mazishi ya marehemu Marie-Celina Kisesa Seme, aliyekuwa mkazi wa Ilala Misheni, Kota Magira Na. 11, jijini Dar es Salaam.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Sinza, ambapo Spika Zungu ametoa salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, akiwataka kupata nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Katika salamu zake za pole, amewaombea wafiwa wawe na uvumilivu na faraja ya Mungu wanapopitia kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.
Amehitimisha kwa kukumbusha maneno ya maandiko matakatifu: “Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe.”







0 Comments