Na Victor Masangu,Kibaha
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt.Samis Suluhu Hassan kuboresha sekta ya elimu ameahihidi kuchangia matofali elfu mbili pamoja na kutoa shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Mwambisi.
Mbunge Koka ameamua kuchangia matofali hayo na kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuweza kuchochea zaidi katika kuboresha sekta ya elimu ili wanafunzi na walimu waweze waweze kuwa katika mazingira ambayo ni rafiki ikiwa sambamba na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Koka amechangia ujenzi wa fedha wakati wa mahafali ya 11 ya Shule ya Sekondari Mwambisi iliyopo Kata ya Kongowe katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha .
Kokw amesema kuwa ili wanafunzi waweze kupata masomo katika mazingira mazuri wadau wanapaswa kuchangia maendeleo ya elimu.
"Mchango uwe chachu ya kufanikisha ujenzi wa mabweni hayo ili wanafunzi wawe kwenye mazingira mazuri,"amesema Koka.
Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Mwambisi Philemon Fredy amesema kuwa wanashukuru mchango huo kwani utasaidia kuanza ujenzi wa mabweni ambayo tunatarajia kuyajenga.
Fredy amesema kuwa wanatarajia kuanza ujenzi hivi karibuni kwani baadhi ya vifaa tayari wanavyo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mabweni manne kwa ajili ya ujenzi.
Baadhi ya michango iliyochangwa ni tofali 2,500 saruji mifuko 33 hivyo kufanya michango yote kuwa na gharama ya shilingi milioni tatu



0 Comments