Na Victor Masangu,Kibaha
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Walda Maulid ameahidi kushirikiana bega kwa bega na Umoja wa wanawake wa (UWT) Wilaya ya Kibaha mji katika kuwakomboa kiuchumi kupitia fursa za mikopo ya asilimia 10.
Hayo ameyabainisha wakati alipokuwa mgeni rasmi wakati wa baraza la dharura ambalo liliandaliwa kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali ikiwemo na suala la kumkaribisha rasmi na mkurugenzi huyo mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
Amesema kwamba kupitia mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa na Halmashauri inawafikia walengwa wote hususan katika kundi la wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi.
"Nimefarijika sana kualikwa katika kikao hiki cha baraza la UWT Wilaya ya Kibaha mjini na mimi nitakuwa pamoja nanyi katika kuhakikisha kwamba mikopo ambayo inatolewa inawafikia kwa ajili ya kuweza kuanzisha biashara mbali mbali,"amebainisha Walda.
Aidha Mkurugenzi huyo amemshukuru kwa dhati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kumteuwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kuahidi kutomwangusha katika kutimiza majukumu yake.
Naye Mwenyekiti wa UWT Elina Mgonja amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuweza kuahidi kuwasaidia kwa hali na mali wanawake hao waweze kujikwamua kiuchumi kupitia fursa za mikopo inayotolewa na Halmashauri.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani Aziza Omary amewahimiza wanawake kuachana na vitendo vya kuwa na migogoro na mipasuko na badala yake waungane katika kukijenga chama na jumuiya zake.
Awali akitoa salamu za jumuiya hiyo Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Cesilia Ndalu amesema kwamba amefarijika kuona Mkurugenzi huyo kuamua kuwaunga mkono wanawake katika suala zima la kuleta maendeleo.
Diwani wa kata ya picha ya Ndege Grace Jungulu ameahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na mkurugenzi huyo mpya kwa lengo kuweza kuwaleta maendeleo wananchi katika maeneo mbali mbali.
Kikao cha baraza hilo la dharura la UWT Wilaya ya Kibaha mji kimekwenda sambamba na halfa fupi ya ya kuweza kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.





0 Comments