Kumuua Baba yake Mzazi na Kumjeruhi Mama yake kwa madai ya kuingilia ugomvi wa Mke wake.




Kijana Athumani Hamis wa Kijiji cha Chingungwe Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara amejikuta mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa Tuhuma za Kumuua Baba yake Mzazi na Kumjeruhi Mama yake kwa madai ya kuingilia ugomvi wa Mke wake.

Chanzo cha ugomvi huo inadaiwa kuwa kwa takribani siku mbili mtuhumiwa huyo, Athumani alimtaka mkewe kufanya naye tendo la ndoa wakati mkewe akiomba kupewa muda na mume wake kwa kuwa afya yake ilikuwa bado haijatengemaa baada ya kujifungua mtoto ambae sasa ana umri wa miezi miwili lakini mumewe hakutaka kumuelewa.
Baada ya kukatiliwa Mama huyo mwenye mtoto mchanga inadaiwa alikimbilia kwa wakwe zake ili kujiepusha na kadhia hiyo na ndipo ugomvi uliibuka nyumbani kwa mzazi wa Athumani.

Post a Comment

0 Comments