Dawasa yaweka mikakati ya kiboresha huduma ya maji kwa wawekezaji


Na Victor Masangu,Pwani 


Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira (DAWASA) imeahidi kuendelea kuboresha na kufikisha huduma ya maji kwa wawekezaji mbali mbali wa viwanda vidogo na vikubwa lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.



Hayo yamebainishwa leo na mtendaji mkuu wa Dawasa Injinia Cyprian Luhemeja wakati akitoa taarifa kwa Rais mstaafu wa awamu  ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Dawasa wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya tatu ya uwekezaji na biashara Mkoa wa Pwani.


Alisema kwamba lengo lao kubwa ni kuweza kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani ikiwemo wawekezaji wa viwanda vyote kuwapatia huduma ya maji.


"Tumeshiriki katika maonesho haya kwa lengo la wananchi waweze kufahamu utekelezaji wa majukumu yetu mbali  mbali ambayo tumekuwa tukiyafanya katika mikoa ya yetu ya Dar es Salaam pamoja na Pwani na tunawahidi kuwaboreshea huhuma ya maji kuanzia ngazi za vitongoji,"alisema Luhemeja.

Post a Comment

0 Comments