WIZARA YA AFYA YAANZA KUTOKOMEZA RASMI MAGONJWA YA MATENDE,MABUSHA IKIWEMO MKOA WA DAR ESALAM.

 

Na Sheila Ahmadi

Wizara ya Afya imeelekeza hatua ambazo zimeweza kufanikiwa katika kutokomeza magonjwa ya Matende na mabusha nchini ikiwemo mkoa wa Dar es salam ambapo halmashauri zenye maambukizi mapya ikiwemo maeneo ya Pangani,Mafia, Kinondoni,kilwa,Lindi manispaa Mtama na Mtwara mikindani.


Akizungumza Jijini Dar es salaam Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa upande wa dar es salam mnamo mwezi march na Agosti mwaka 2023 na mwaka 2024 February wizara ya Afya kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa tumeweza kufanya Tathmini za viwango vya maambukizi ya ugonjwa wa matende na mabusha kutoka kwenye halmashauri.


Tunaendelea na zoezi la kampeni za umezeshaji wa kingatiba ya ugonjwa wa matende na mabusha katika kata kumi za manispaa ya kinondoni zikiwemo Tandale,kijitonyama,Mwananyamala,kigogo,,Mzimuni  Magomeni,makumbusho na Hananasifu hivyo zoezi hili litaendelea anagalau kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo kabla ya kurudia  tena kufanya tathmini.


"Natoa rai kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salam hususani kutoka kata za kigogo na mwananyamala ambapo bado kuna maambukizi ya ugonjwa huu amabo umejitokeza kwa wingi ili kushiriki kwenye kampeni za kingatiba ya ugonjwa huo wa matende na mabusha ambazo zitaendelea kufanyika kwenye maeneo yao ili kuweza kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo " Amesema waziri Ummy.


Aidha kupitia tathimini hizo ni faraja kwetu kuona kuwa tumefanikiwa kuwanusuru wananchi zaidi ya million 3.7 katika kuwaepusha na hatari ya kupata maambukizi ya vimelea vya ugonjwa wa matende na mabusha.


Ninamshukuru  Mh Dkt samia suluhu hasani Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuunga mkono jitihada za kutokomeza magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele ambapo kupitia mkutano wa Reaching the last mile uliofanyika mwezi disemba mwaka 2023 huko Dubai.


Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wote kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana  na ugonjwa huu ili kwenda kuhakikisha ugonjwa huu unatokomezwa ifikapo mwaka 2030

Post a Comment

0 Comments