Na' Mwandishi Wetu.
Maandamano ya amani ya Bawacha ambayo yaliyopangwa kufanyika siku ya leo tarehe 9 May 2023 kwa lengo la kumshikinikiza spika wa bunge la JMT, awaondoea Bungeni wabunge 19 wa Vitimaalum CHADEMA yamezuiwa na Jeshi la Polisi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Makao makuu wa CHADEMA kinondoni Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Bawacha Taifa Catherine Ruge amesema Jeshi la Polisi limezia maandamano hayo kwa kile walichodai kulikuwa na makosa ya uwasilishaji wa barua hiyo ya kuomba kufanyika maandamano kwenye Ofisi ambayo haina mamlaka.
"Mkuu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ametueleza kuwa tumefanya makosa kupeleka barua katika ofisi yake na badala yake tulipaswa kupeleka kwa Mkuu wa polisi wa wilaya ya Ilala kwa maana ya OCD masaa 48 kabla ya Maandamano"
BAWACHA wanaeleza barua ya kwanza kabisa waliipeleka kwa OCD wa Ilala siku ya tarehe 5 May 2023 nakuambiwa waipeleke kwa RPC, ndipowalipofanya mabadiliko kuipeleka barua hiyo kwa RPC.
Hatalivyofika ofisi ya RPC waliatambiwa tunapaswa kupeleka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maaalum, na kuelekezwa namba ya kuandika nanuani na Msaidizi wa afande Muliro na kaandika juu ya barua.
Baada ya marekebisho ndipo barua ikapekekwa tena kwa ofisi ya Kanda Maalum Dar es Salaam , na ikapokelewa na kupewa nakala.
"Jukumu letu ni kutoa taarifa na sio kuomba kibali, na kwa kuwa maandamano yetu ni ya amani, polisi wanaweza kuendelea na majukumu yao wasipoteze muda na rasirimali kuja kutulinda Bawacha."
"Pia polisi wametushauri tuachane na maandamano kwa kuwa jambo hili liko Mahakamani, sisi Bawacha tumekataa ushauri wao tutaendelea na Maandamano siku ya alhamis tarehe 11May, hivyo basi tunaliomba jeshi la Polisi liendelee kutimiza wajibu wake na sisi mtuache tutimize wajibu wetu wa Kikatiba kama chama cha siasa."

0 Comments