RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI TANZANIA*

 




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe. Kyle Nunas aliyefika Ikulu Zanzibar leo tarehe 03 Mei 2023.


Katika mazungumzo hayo Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali umewekeza katika sekta ya afya na elimu ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora hasa vijijini. Pia, Serikali  inazingatia kukuza huduma ya afya ya kinga kwa mama na mtoto na mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza.


Aidha, Serikali imeweka kipaumbele cha kujenga uwanja mpya wa ndege (Terminal 4) ili kuimarisha miundombinu hususan inayohusiana na utalii, ambapo ndio  sekta muhimu ya uchumi Zanzibar.


📅 03 Mei 2023


📍Ikulu ,Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments