Waziri wa Nishati January Makamba amesema kuwa kumekuwa na hoja na mjadala kwabaadhi ya wanasiasa hasa wa upande wapili wakidai mwenge wa uhuru umepitwa na wakati.
Makamba amesema kuwa Mwenge ni Tunu ni nembo ya Taifa hivyo na kwa
kusema mwenge unasumbua watu ni sawa na kuitusi nchi ya Tanzania.
Makamba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Bumbuli ameyasema hayo mara baada
ya mwenge kufika katika Jimbo hilo, ambapo mwenge huo umezindua na
kukagua miradi 9 yenye thamani ya sh.779.1 million
" Tukiwa na mawazo na mtazamo huo tunaitusi historia ya nchi yetu
kwani nchi yetu ilipopata uhuru, hotuba ya kwanza ya Baba wa Taifa
Mwalimu Nyerere amesema sasa tunawasha mwenge iliuangaze nchinzima, "
amesema January Makamba
Alisisitiza kuwa mwenge wa uhuru ni kielelezo cha uhuru, utaifa wetu,
ni ndoto zetu, na ni kiunganishi cha watanzania pamoja na kuwa
utamaduni na kielelezo cha utaifa wa Tanzania.
Alifafanua kuwa kila nchi ina urithi wake na utamaduni zake na kila ukoo
una tamaduni zake na kwamba kwa Tanzania moja ya urithi wake ni Mwenge
na ndiyo maana upo kwenye nembo ya taifa na hata kwenye sarafu.
0 Comments